Makundi ya Wazayuni yatishia kumuua mrithi mtarajiwa wa Netanyahu, Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i70954-makundi_ya_wazayuni_yatishia_kumuua_mrithi_mtarajiwa_wa_netanyahu_israel
Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni wa Israel vimetangaza kuwa, waziri mkuu mtarajiwa wa utawala huo Naftali Bennett anayetoka muungano wa wapinzanii wa waziri mkuu wa ssaa Benjamin Netanyahu ametishiwa kuuawa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 06, 2021 02:57 UTC
  • Makundi ya Wazayuni yatishia kumuua mrithi mtarajiwa wa Netanyahu, Israel

Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni wa Israel vimetangaza kuwa, waziri mkuu mtarajiwa wa utawala huo Naftali Bennett anayetoka muungano wa wapinzanii wa waziri mkuu wa ssaa Benjamin Netanyahu ametishiwa kuuawa.

Televisheni ya Israel imetangaza kuwa, vyombo vya usalama vya utawala huo vimesema, vimepokea ripoti ya vitisho vya kuuliwa kiongozi wa chama cha New Right, Naftali Bennett, na kwamba vinafuatilia ipasavyo suala hilo.   

Awali Jenerali Nadav Argaman mkuu wa Shirika la Usalama wa Ndani la Israel (Shin Bet) alikuwa tayari ametahadharisha kuhusu mpango wa kuuawa viongozi wa kisiasa wa utawala huo kufuatia kuungana vyama vya mrengo wa kulia, vile vya mrengo wa kati na vya kushoto kwa ajilii ya kumuondoa madarakani Benjamin Netanyahu na kuunda serikali mpya. 

Itakumbuka pia kwamba wafuasi wa Benjamin Netanyahu hivi majuzi walikusanyika mbele ya ofisi ya Yair Lapid, kiongozi wa chama cha upinzani cha Yesh Atid wakipinga jaribio lolote la kundwa serikali mpya. 

Jumatano iliyopita Yair Lapid alimtaarifu Rais wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Reuven Rivlin kwamba yuko tayari kuunda serikali mpya baada ya aliyekuwa waziri mkuu wa utawala huo Benjamin Netanyahu kushindwa kuunda baraza jipya la mawaziri.