Yemen: UN inafumbia macho uharamia wa Saudia na washirika wake
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i73986-yemen_un_inafumbia_macho_uharamia_wa_saudia_na_washirika_wake
Shirika la Mafuta la Yemen limeukosoa Umoja wa Mataifa kwa kunyamazia kimya na kufumbia macho uharamia unaoendelea kufanywa na wavamizi wa Yemen wanoongozwa na Saudi Arabia, suala ambalo linazidisha mgogoro wa raia wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 27, 2021 06:46 UTC
  • Yemen: UN inafumbia macho uharamia wa Saudia na washirika wake

Shirika la Mafuta la Yemen limeukosoa Umoja wa Mataifa kwa kunyamazia kimya na kufumbia macho uharamia unaoendelea kufanywa na wavamizi wa Yemen wanoongozwa na Saudi Arabia, suala ambalo linazidisha mgogoro wa raia wa nchi hiyo.

Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa na Shirika la Mafuta la Yemen imesema kuwa, tangu mwanzoni mwa mwaka huu muungano vamizi unaoongozwa na Saudia umezuia meli zinazobeba nishati kuelekea Yemen na kuruhusu meli tatu tu zinazobeba asilimia 3 ya petroli na asilimia 6 ya mafuta ya taa yanayohitajiwa kwa sasa na watu wa Yemen. 

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, Saudi Arabia na washirika wake wametwaa meli nne zinazobeba nishati licha ya kuwa na kibali cha kimataifa na kwamba gharama ya kusitishwa shehena hiyo ya nishati inakadiriwa kufikia zaidi ya dola milioni 6.

Shirika la Mafuta la Yemen limetoa wito wa kuzidishwa mashinikizo dhidi ya Saudia na washirika wake katika uvamizi wa ardhi ya Yemen ili zikomeshe wizi na uharamia huo na athari zake mbaya kwa watu wa Yemen. Vilevile limewataka watu wote huru duniani kuishikiza Saudia na waitifaki wake ili waache kutumia silaha ya mzingiro na njaa dhidi ya watu wa Yemen. 

Yemen inasumbuliwa na ukosefu mkubwa wa nishati, chkula, dawa na zana za tiba kwa mwaka wa sita sasa kutokana na mzingiro wa baharini, nchi kavu na angani wa Saudia na Washirika wake.

Hali ya watoto wa Yemen

Viongozi wa Yemen wanasisitiza kuwa kuzuia chakula, dawa, vifaa vya tiba na nishati kwa watu wa Yemen ni mauaji ya umati ya kizazi na kwamba mamilioni ya watoto wanaosumbuliwa na magonjwa ya aina mbalimbali nchini humo wanakabiliwa na hatari ya kifo kutokna na mzingiro huo wa kinyama.