WHO yatahadharisha kuhusu akiba ya misaada ya matibabu Afghanistan
Umoja wa Mataifa umetahadharisha juu ya kukaribia kumalizika misaada ya matibabu huko Afghanistan.
Rick Brennan Mkurugenzi wa Ofisi ya Kikanda ya Oparesheni za Dharura za Shirika la Afya Duniani yeney makao yake mjini Cairo Misri jana alitangaza katika mkutano na waandishi wa habari kuwa, akiba ya misaada ya kitiba ka huko Afghanistan inakaribia kumalizika na kwamba hatua za haraka zinapasa kuchukuliwa.
Mkurugenzi huyo wa Kikanda wa Oparesheni za Dharura wa WHO ameongeza kuwa: wanatafuta mbadala wa uwanja wa ndege wa Kabul kwa kuzingatia hali ya kilojistiki na pia ya usalama inayoshuhuiwa sasa huko Afghanistan.
Rick Brennan ambaye ameeleza haya siku moja baada ya kujiri milipuko karibu na milango mikuu ya kuingilia uwanja wa ndege wa Kabul amebainisha kuwa; gharama za bima ya kusafiri kuelekea Afghanistan imeongezeka pakubwa. Afisa huyo wa WHO amesema kuwa anataraji kuwa katika muda wa masaa 48 hadi 72 yajayo mazingira ya safari za ndege kuelekea Afghanistan yataandaliwa.
Milipuko miwili mmoja uliotokea karibu na uwanja wa ndege wa Kabul na mwingine katika Hoteli ya Baron umeuwa watu 103 wakiwemo raia 90 wa Kiafghani na wanajeshi vamizi wa Marekani 13. Makumi ya watu pia wamejeruhiwa katika mlipuko huo.