Iran itafuatilia kisheria na kimataifa kadhia ya makamanda waliouawa shahidi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i74020-iran_itafuatilia_kisheria_na_kimataifa_kadhia_ya_makamanda_waliouawa_shahidi
Wazari wa Mambo ya Nje wa Iran amesema wizara yake itafuatilia kisheria na kimataifa kadhia ya makamanda wa muqawama waliouawa shahidi katika hujuma za kigaidi ambao ni Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na Abu Mahdi Muhandes, Kamanda wa Kikosi cha Hashd Shaabi cha Iraq.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 28, 2021 11:31 UTC
  • Iran itafuatilia kisheria na kimataifa kadhia ya makamanda waliouawa shahidi

Wazari wa Mambo ya Nje wa Iran amesema wizara yake itafuatilia kisheria na kimataifa kadhia ya makamanda wa muqawama waliouawa shahidi katika hujuma za kigaidi ambao ni Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na Abu Mahdi Muhandes, Kamanda wa Kikosi cha Hashd Shaabi cha Iraq.

Hussein Amir-Abdollahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameyasema hayo leo asubuhi katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege mjini Baghdad, Iraq wakati alipotembelea eneo walipouawa makamanda hao  wawili. Akijibu swali la mwandishi habari amesema, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran inafuatilia kisheria na kimataifa kadhia ya mauaji ya makamanda hao wawili ambao waliuawa kigaidi kufuatia amri ya serikali ya Marekani.

Amesema: "Ni lazima Marekani itoe jibu hata kama jinai hiyo ilitendwa na serikali iliyopita," na kuongeza kuwa wale waliotenda jinai hiyo ya kigaidi ni lazima wafikishwe kizimbani kujibu mashtaka.

Mashahidi Qassem Soleimani  (kushoto) na Abu Mahdi Muhandis

Hussein Amir-Abdollahian leo amefika Baghdad katika safari yake ya kwanza ya nje ya nchi baada ya kuteuliwa na rais na kisha kuidhinishwa na bunge kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.  Akiwa nchini Iraq atashiriki katika  'Kongamano la Usalama la Baghdad' ambalo linafanyika leo na kuhudhuriwa na wawakilishi wa nchi zinazopakana na Iraq na pia baadhi ya viongozi wa nje ya eneo.