Wasyria walalamikia hatua ya Marekani kuunga mkono ISIS
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i74052-wasyria_walalamikia_hatua_ya_marekani_kuunga_mkono_isis
Wasyria kutoka kabila la Shaitat wamefanya maandamano katika Jimbo la Dayr al-Zawr Mashariki kulaani hatua ya Marekani ya kuwakamata watu 300 wa kabila hilo ambalo walikuwa wanakabiliana na kundi la kigaidi la ISIS au Daesh.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 29, 2021 03:26 UTC
  • Wasyria walalamikia hatua ya Marekani kuunga mkono ISIS

Wasyria kutoka kabila la Shaitat wamefanya maandamano katika Jimbo la Dayr al-Zawr Mashariki kulaani hatua ya Marekani ya kuwakamata watu 300 wa kabila hilo ambalo walikuwa wanakabiliana na kundi la kigaidi la ISIS au Daesh.

Washiriki wa maandamano hayo ya Jumamosi wametaka kuachiliwa kwa watu wa kabila hilo, ambao wanashikiliwa katika magereza yanayoendeshwa na wanaomgambo wa Kikurdi wanaojiita Vikosi vya Kidemokrasia vya Siria (SDF), ambao wanaungwa mkono na Marekani. Wanamgambo hao wa SDF wako vitani dhidi ya serikali halalai ya Syria.

Waandamanaji hao wamenukuliwa na Shirika la Habari la Sputnkik wakisema wanajeshi wa Marekani na wanamgambo wa SDF wamewafunga jela watu wa ukoo wa Shaitat bila mashtaka yoyote.

Wametishia kwamba ikiwa wafungwa hawataachiliwa, maandamano yataenea kote Dayr al-Zawr.

Wakati huo huo, shirika rasmi la habari la SANA la Syria limeripoti kuwa waandamanaji walifunga barabara zinazoelekea Abu Hamam kwa kuchoma matairi.

Wanamgambo wa SDF wanaopata himaya ya Marekani nchini Syria

Syria imekuwa ikikabiliana na magaidi na wanamgambo wanaoungwa mkono na madola ajinabi tokea Machi 2011. Serikali ya Syria inasema Marekani na washirika wake wanasaidia vikundi vya kigaidi na Kitakfiri ambavyo vimeleta maafa katika nchi hiyo ya Kiarabu.

Marekani imepeleka vikosi na vifaa vya kijeshi nchini Syria bila idhini yoyote kutoka Damascus au Umoja wa Mataifa. Kwa muda mrefu imekuwa ikiwapatia mafunzo wanamgambo na kuiba mafuta ya Syria, ikipuuza wito wa Damascus wa kuacha kuikalia ardhi ya nchi hiyo kwa mabavu.