Wamarekani waiba shehena nyingine ya mafuta ya Syria
(last modified Wed, 15 Sep 2021 06:21:03 GMT )
Sep 15, 2021 06:21 UTC
  • Wamarekani waiba shehena nyingine ya mafuta ya Syria

Wanajeshi magaidi na wavamizi wa Marekani wameiba shehena nyingine ya mafuta ya wananchi wa Syria.

Shirika la habari la SANA limeripoti habari hiyo na kuiongeza kuwa, wanajeshi vamizi wa Marekani wanaendelea kuiba mafuta na rasilimali ya Syria huku shehena ya karibuni kabisa ya mafuta ya nchi hiyo waliyoiiba wanajeshi magaidi wa Marekani ni ile ya jana Jumanne. Wanajeshi hao wametumia magani ya deraya na zana kubwa za kijeshi kuiba mafuta hayo kutoka al Hasaka Syria na kuyapeleka nchini Iraq.

Duru za eneo hilo zimesema kuwa, zimeona msafara mkubwa wa magari yafikayo 70 yakiwemo malori ya kubebea mafuta ya wizi yakivuuka mpaka wa Syria na kuingia Iraq kwa ulinzi mkali wa wanajeshi vamizi na magaidi wa Marekani. 

Wanajeshi magaidi wa Marekani wakiwa kwenye visima vya mafuta vya Syria

 

Kabla ya hapo Basam Tohme (بسام طعمه), Waziri wa Mafuta wa Syria alikuwa amesema kuwa, asilimia 90 ya akiba na utajiri wa mafuta wa nchi hiyo iko katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Marekani. Si hayo tu, lakini pia wanajeshi magaidi wa Marekani na mamluki wao mara kwa mara wanashambulia malori ya mafuta ya Syria.

Mwaka 2017, Syria ilifanikiwa kuwasambaratisha magaidi wa Daesh (ISIS) ambao walikuwa wanatumiwa na Marekani kufanya mauaji, jinai, kuhalalisha uingiliaji wa kigeni na kupora utajiri wa nchi hiyo ya Kiarabu.

Hata hivyo dhati ya dola la kibeberu la Marekani ni wizi na uporaji na ndio maana hivi sasa linatumia mamluki wengine kuiba na kupora utajiri wa Syria bila ya kificho.