Muungano vamizi wa Saudi Arabia washambulia maeneo mbalimbali ya Yemen
Ndege za kijeshi za muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia zimefanya hujuma na mashambulio ya anga dhidi ya maeneo mbalimbali ya Yemen.
Ripoti kutoka Yemen zinasema kuwa, jana ndege za kivita za muuungano vamizi wa Saudi Arabia zimefanya mashambulio mara nane katika mji wa Sarwah na mara sita dhidi ya mji wa al-Jawbah katika mkoa wa Ma'rib.
Aidha miji mingine kadhaa ya Yemen jana iliandamwa kwa mashambulio ya mabomu ya muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia ukiwemo mkoa wa Sa'da na Uwanja wa Ndege wa Taizz.
Watu kadhaa wanaripotiwa kuuawa na kujeruhiwa katika mashambulio hayo huku kukishuhudiwa uharibu mkubwa wa nyumba na mali za watu.
Hujuma na mashambulio hayo ya Saudia na washirika wake yanaendelea licha ya kuweko miito ya kieneo na kimataifa inayotaka kusitishwa mauaji hayo dhidi ya wananchi wa Yemen.

Wakati huo huo shirika moja la kutetea haki za binadamu limesema mamia ya watoto wa Yemen wanafariki dunia ndani ya kila saa 24 kutokana na utapiamlo, huku muungano wa kivita unaoongozwa na Saudi Arabia ukiendelea kufanya mashambulizi na kuliwewekea mzingiro wa kila upande taifa hilo maskini la Kiarabu.
Kufuatia uungaji mkono wa Marekani, Imarati, utawala haramu wa Israel na nchi nyingine kadhaa za Kiarabu, Saudi Arabia iliivamia kijeshi nchi masikini ya Yemen mnamo Machi 2015 na kuiwekea mzingiro wa pande zote wa nchi kavu, anga na majini. Uvamizi wa kijeshi wa Saudia umeisababishia pia nchi masikini ya Yemen uhaba mkubwa wa chakula na dawa.