Waziri Mkuu wa Iraq: Wanajeshi wa Marekani lazima waondoke
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i77952-waziri_mkuu_wa_iraq_wanajeshi_wa_marekani_lazima_waondoke
Waziri Mkuu wa Iraq amesisitiza kuwa, suala la kuondoka wanajeshi wa Marekani nchini humo haliepukiki na kwamba jambo hilo litaanza karibuni hivi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 12, 2021 08:26 UTC
  • Wanajeshi magaidi wa Marekani nchini Iraq
    Wanajeshi magaidi wa Marekani nchini Iraq

Waziri Mkuu wa Iraq amesisitiza kuwa, suala la kuondoka wanajeshi wa Marekani nchini humo haliepukiki na kwamba jambo hilo litaanza karibuni hivi.

Mustafa al Kadhimi amesema hayo na kuongeza kuwa, siku chache zijazo, wanajeshi wote wapiganaji wa Marekani wataondoka katika ardhi ya Iraq kama ilivyokubaliwa kwenye mapatano ya nchi hizo mbili. 

Amesema, watakaobakia nchini Iraq watakuwa ni washauri wa kijeshi tu wa Marekani na hilo linaonesha kwamba vikosi vya ulinzi vya Iraq vina uwezo wa kutosha wa kulinda usalama wa taifa hilo.

Wakati huo huo, Matthew Tueller, balozi wa Marekani nchini Iraq amesema wakati alipoonana na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Mustafa al Kadhimi kwamba, Iraq ni nchi yenye umuhimu mkubwa kwa usalama na utulivu wa eneo hili.

Waziri Mkuu wa Iraq, Mustafa al Kadhimi

 

 

Tarehe 26 Julai mwaka huu, Baghdad na Washingon zilifikia makubaliano ya kuhakikisha kuwa wanajeshi wa Marekani wanaondoka nchini Iraq ifikapo mwishoni mwa mwaka huu wa 2021.

Mwaka 2014 Marekani ilituma wanajeshi 3000 nchini Iraq kwa madai ya kushiriki katika operesheni za eti muungano wa kimataifa wa kupambana na Daesh yaani ISIS. 

Hata hivyo baada ya kutangazwa ushindi dhidi ya Daesh na kusambaratishwa magaidi hao - ambao tangu kuanzishwa kwa magenge yao hadi kupata nguvu na kuteka maeneo mengi ya Iraq, walifanya hivyo kwa msaada wa mabeberu wa dunia ikiwemo Marekani - sasa hivi tena Marekani haina kisingizio kingine chochote cha kubakisha wanajeshi wake magaidi huko Iraq.