Israel yashambulia kwa makombora mashariki mwa Qunaitra, kusini mwa Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i80668-israel_yashambulia_kwa_makombora_mashariki_mwa_qunaitra_kusini_mwa_syria
Duru za habari nchini Syria zimetangaza kuwa, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wameshambulia kwa makombora maeneo ya karibu na mji wa Qunaitra nchini Syria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 23, 2022 03:42 UTC
  • Israel yashambulia kwa makombora mashariki mwa Qunaitra, kusini mwa Syria

Duru za habari nchini Syria zimetangaza kuwa, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wameshambulia kwa makombora maeneo ya karibu na mji wa Qunaitra nchini Syria.

Shirika la habari la IRIB limetangaza habari hiyo leo asubuhi na kuongeza kuwa, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wameshambulia kwa makombora kadhaa maeneo ya mji huo wa kusini mwa Syria ambao unapakana na milima ya Golan ya Syria inayokaliwa kwa mabavu na utawala pandikizi wa Israel.

Duru za eneo hilo nazo zimethibitisha habari hiyo na kusema kuwa, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wamefanya shambulio hilo katika kijiji kimoja kilichoko karibu na eneo linalotangenisha maeneo ya Syria na yale yanayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni katika milima hiyo ya Golan.

Milima ya Golan ya Syria inayokaliwa kwa mabavu na Israel

 

Muda wote utawala wa Kizayuni wa Israel umekuwa ukiyasaidia magenge ya kigaidi yanayofanya mauaji dhidi ya raia wa Syria na maafisa wa serikali ya nchi hiyo. Kila magenge hayo ya kigaidi yanapozidiwa nguvu, wanajeshi magaidi wa Israel huyasaidia kupitia kufanya mashambulio kama hayo.

Jambo linalowatia wahka mkubwa Wazayuni wavamizi ni kuundika muqawama wa watu wa maeneo ya Golan kwa ajili ya kuikomboa milima hiyo ya Syria inayokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni hasa kwenye mji wa Qunaitra.

Mara kwa mara serikali ya Syria imekuwa ikilalamikia jinai hizo za Israel na imekuwa ikiuandikia barua Umoja wa Mataifa kuushitaki utawala wa Kizayuni hata kama umoja huo hauchukui hatua yoyote ya maana.