Wazayuni wasiopungua wanne waangamizwa katika operesheni ya Wapalestina ya Bi'ru-Sab'i
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i81694-wazayuni_wasiopungua_wanne_waangamizwa_katika_operesheni_ya_wapalestina_ya_bi'ru_sab'i
Duru za Palestina zimeripoti kuwa Wazayuni wasiopungua wanne wameangamizwa katika operesheni ya muqawama iliyotekelezwa na kijana Mpalestina katika mji wa Bi'ru-Sab'i Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan.
(last modified 2026-08-08T07:03:00+00:00 )
Mar 23, 2022 03:30 UTC
  • Wazayuni wasiopungua wanne waangamizwa katika operesheni ya Wapalestina ya Bi'ru-Sab'i

Duru za Palestina zimeripoti kuwa Wazayuni wasiopungua wanne wameangamizwa katika operesheni ya muqawama iliyotekelezwa na kijana Mpalestina katika mji wa Bi'ru-Sab'i Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan.

Mji wa Bi'ru-Sab'i jana ulishuhudia operesheni ya muqawama iliyotekelezwa na Shahidi Muhammad Ghalib Abul-Qaian.

Askari katili wa utawala dhalimu wa Kizayuni, kila siku wanatumia visingizio tofauti kuwashambulia na kuwaua shahidi au kuwajeruhi na kuwatia nguvuni wananchi madhulumu wa Palestina; kwa sababu hiyo, wananchi hao nao wanatekeleza operesheni za muqawama kujibu jinai hizo wanazofanyiwa na Wazayuni.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRIB, Muhammad Ghalib Abul-Qaian, ndiye aliyetekeleza operesheni ya muqawama ya jana jioni katika mji wa Bi'ru-Sab'i kwa kutumia kisu na kufanikiwa kuwaangamiza wazayuni wasiopungua wanne.

Vyombo vya habari vya Palestina vimetangaza kuwa, askari wa Kizayuni walimuua shahidi kwa kumpiga risasi kijana huyo.

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS jana hiyohiyo ilitoa mkono wa hongera kwa operesheni ya muqawama katika mji wa Bi'ru-Sab'i na kusisitiza kuwa mapambano ya Wapalestina ya kukabiliana na Wazayuni maghasibu yangali yanaendelea na hali ya mapigano iliyopo haitasitishwa kamwe.

Harakati ya Jihadul-Islami nayo pia imesifu na kupongeza operesheni ya Bi'ru-Sab'i na kusisitiza kwamba ni muqawama pekee ndio utakaowafanya Wazayuni maghasibu waache kuendeleza uvamizi na uchokozi.

Baada ya kutekelezwa operesheni hiyo ya kishujaa, kundi kubwa la askari wa Kizayuni lilikwenda kuvamia nyumbani kwao Shahidi Muhammad Ghalib  Abul-Qaian katika eneo la Hawr, huko An-Naqb.../