Alqaida na ISIS watwangana, wanamapambano wa Yemen wakomboa maeneo muhimu Ma'rib
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i81730-alqaida_na_isis_watwangana_wanamapambano_wa_yemen_wakomboa_maeneo_muhimu_ma'rib
Duru za Yemen zimetangaza habari ya kutokea mapigano makali baina ya makundi ya kigaidi kusini mwa mkoa wa Ma'rib huku wanamapbamano wa Yemen wakikomboa baadhi ya maeneo muhimu ya kiistratijia katika mkoa huo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 24, 2022 02:41 UTC
  • Alqaida na ISIS watwangana, wanamapambano wa Yemen wakomboa maeneo muhimu Ma'rib

Duru za Yemen zimetangaza habari ya kutokea mapigano makali baina ya makundi ya kigaidi kusini mwa mkoa wa Ma'rib huku wanamapbamano wa Yemen wakikomboa baadhi ya maeneo muhimu ya kiistratijia katika mkoa huo.

Makundi hayo ya kigaidi ni ya mamluki wa muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) na taarifa za uhakika zinasema ni baina ya magaidi wa al Qaida na Daesh yaani ISIS.

Shirika la habari la Tasnim limezinukuu duru za kieneo mkoani Ma'rib zikisema kuwa mapigano hayo makali baina ya mtandao wa kigaidi wa al Qaida na genge la wakufurishaji la Daesh, yametokea kwenye viunga vya Wadi Ubaidah, kusini mwa mji wa Ma'rib.

Vita vya ukombozi wa Ma'rib nchini Yemen

 

Duru hizo zimeongeza kuwa, makundi ya kigaidi yanaendelea kupigana yenyewe kwa yenye na hadi inaripotiwa habari hii, magaidi kadhaa walikuwa wameangamizwa na wengine wengi kujeruhiwa. 

Hayo yameripotiwa huku Waziri wa Ulinzi wa Serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen yenye makao yake mjini Sana'a, Muhammad al Aatifi akiwa amesema kuwa, mwaka wa nane wa muqawama na kusimama imara wananchi wa Yemen, ni mwaka wa dhoruba na tufani za Yemen, wa mafanikio makubwa ya silaha za kisasa za kistratejia na ni mwaka wa uchukuaji hatua kali na madhubuti zaidi za kuzuia hujuma dhidi ya nchi hiyo.

Al Atifi amesema: "leo sisi tumo katika kupiga hatua thabiti zaidi mbele kwa ajili ya kupata mafanikio mapya ya kijeshi, ambayo yatakuwa ya kustaajabisha; mafanikio ambayo yatageuza mlingano wa nguvu."