Barabara za Ghaza zapambwa kusubiri Siku ya Kimataifa ya Quds
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i83018-barabara_za_ghaza_zapambwa_kusubiri_siku_ya_kimataifa_ya_quds
Huku Ijumaa ya kesho ya tarehe 29 Aprili mwaka ikiwa ni Siku ya Kimataifa ya Quds yaani Ijumaa ya mwisho ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani, tayari mitaa ya Ukanda wa Ghaza imepambwa kwa picha mbalimbali za mashahidi wa kambi ya muqawama ya ukombozi wa Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 28, 2022 02:36 UTC
  • Barabara za Ghaza zapambwa kusubiri Siku ya Kimataifa ya Quds

Huku Ijumaa ya kesho ya tarehe 29 Aprili mwaka ikiwa ni Siku ya Kimataifa ya Quds yaani Ijumaa ya mwisho ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani, tayari mitaa ya Ukanda wa Ghaza imepambwa kwa picha mbalimbali za mashahidi wa kambi ya muqawama ya ukombozi wa Palestina.

Imam Khomeini MA, mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliitangaza Ijumaa ya mwisho ya kila mwezi wa Ramadhani kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds kwa lengo la kutangaza mshikamano wa dunia nzima kwa kadhia ya Palestina na pia kuyabakisha hai mapambano ya ukombozi wa Kibla cha Kwanza cha Waislamu.

Kama tulivyotangulia kusema, Ijumaa ya kesho ya tarehe 29 Aprili 2022 ndiyo Ijumaa ya mwisho ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani kwa mwaka huu wa 1443 na ndiyo Siku ya Kimataifa ya Quds kwa mwaka huu wa 2022.

Nchini Iraq nako Waislamu wamejiandaa hivi kuipokea Siku ya Kimataifa ya Quds ambayo ni Ijumaa ya kesho Aprili 29, 2022

 

Mtandao wa habari wa al Ahd umeripoti habari hiyo na kusambaza pia picha ya shahid Jihad Mughniya, mtoto wa kiume wa shahid Imad Mughniya ambaye alikuwa miongoni mwa makamanda wakuu wa Hizbullah ya Lebanon pamoja na picha ya Hassan al Qabs mmoja wa viongozi wa Hizbullah pembeni mwa picha za mashahidi wa Ghaza na Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan huku maandishi yake yakiwa ni ujumbe wa Imam Khomeini MA, mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu Quds zikiwa zimebandikwa katika mitaa ya Ghaza.

Maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds hufanyika katika Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kila mwaka katika maeneo na nchi nyingi ulimwenguni. Maadhimisho ya mwaka huu yanatarajiwa kuwa ya hamasa kubwa zaidi kutokana na jinai za kutisha zilizofanywa na wanajeshi makatili wa Israel dhidi ya Waislamu ndani ya Msikiti wa al Aqsa huko Palestina hivi karibuni.