UN yakosoa takwa la kuondolewa Assad madarakani
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i835-un_yakosoa_takwa_la_kuondolewa_assad_madarakani
Kamati ya Kimataifa inayofanya uhakiki kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Syria imetangaza kuwa, msimamo unaosisitiza juu ya udharura wa kuondoka madarakani Rais Bashar Assad kabla ya kuanza mazungumzo ya amani, ni kizuizi katika njia ya kupambana na ugaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 08, 2016 05:53 UTC
  • UN yakosoa takwa la kuondolewa Assad madarakani

Kamati ya Kimataifa inayofanya uhakiki kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Syria imetangaza kuwa, msimamo unaosisitiza juu ya udharura wa kuondoka madarakani Rais Bashar Assad kabla ya kuanza mazungumzo ya amani, ni kizuizi katika njia ya kupambana na ugaidi.

Carla Del Ponte ambaye ni mwanachama wa kamati huru ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa amesema sharti la kushinda vita dhidi ya ugaidi ni kuzidishwa juhudi na ushirikiano wa jamii ya kimataifa na serikali ya Syria na kwamba mjadala wa kuondoka madarakani Rais Bashar Assad kabla ya mazungumzo ya aina yoyote unavuruga jitihada za kupambana na ugaidi. Del Ponte ameongeza kuwa, matokeo ya kung'ang'ania msimamo huo ni kuuliwa zaidi wananchi wa Syria na kuharibiwa kikamilifu nchi hiyo.

Carla Del Ponte amesema kamati yake iko tayari kushirikiana na serikali ya Syria kwa ajili ya kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo na kwamba tayari serikali ya Damascus imemwalika kwenda nchini humo.