Wapalestina waandamana kupinga ziara ya Biden Asia Magharibi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i85894-wapalestina_waandamana_kupinga_ziara_ya_biden_asia_magharibi
Mamia ya Wapalestina wamefanya maandamano katika eneo la kaskazini la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kupaza sauti zao za kupinga ziara ya Rais Joe Biden wa Marekani katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu yaliyopachikwa jina la Israe katika safari yake ya kwanza ya Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) kama rais wa Marekani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 15, 2022 02:48 UTC
  • Wapalestina waandamana kupinga ziara ya Biden Asia Magharibi

Mamia ya Wapalestina wamefanya maandamano katika eneo la kaskazini la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kupaza sauti zao za kupinga ziara ya Rais Joe Biden wa Marekani katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu yaliyopachikwa jina la Israe katika safari yake ya kwanza ya Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) kama rais wa Marekani.

Waandamanaji hao walikusanyika kwenye Uwanja wa Mashahidi mjini Nablus, ulioko takriban kilomita 49 kaskazini mwa al-Quds (Jerusalem), Alhamisi alasiri katika maandamano yaliyoandaliwa na Kamati ya Uratibu ya Makundi ya Palestina.

Wapalestina hao walisikika wakitoa nara dhidi ya Marekani za kupinga safari ya Biden, na kukemea sera za wazi za Washington za kuupendelea utawala ghasibu wa Israel.

Nasser Jawabreh, mjumbe mkuu wa Kamati ya Uratibu wa Makundi ya Palestina alisema katika hotuba yake katika hafla hiyo kwamba taifa zima la Palestina, mirengo na taasisi za kisiasa zinapinga safari ya rais huyo mwenye umri wa miaka 79 kwa vile anaunga mkono wazi wazi utawala bandia wa Israel.

Rais Biden wa Marekani

Wakati huo huo  Bassem Na'aim, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu, Hamas, amesema Rais wa Marekani hana suluhu la mzozo wa Palestina na Israel. Naye Ahmad Al-Medalal, mwanachama wa harakati ya Jihadi ya Kiislamu alisisitiza kwamba Wapalestina hawapaswi kutegemea "mradi wa Marekani katika eneo."

Amesema uongozi wa Palestina lazima uunde safu ya kitaifa ili kukabiliana na utawala wa Israel.

Maher Mezher, kiongozi wa  Chama cha Wananchi kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina (PFLP), pia amesema kuwa ziara ya Biden inalenga kuimarisha ubeberu wa Marekani katika eneo hilo.