Wazayuni wazidi kuwateka nyara wanawake na wasichana wa Kipalestina
Tangu ilipoanza Intifadha ya Quds mwanzoni mwa mwezi Oktoba 2015 hadi hivi sasa, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshawateka nyara makumi ya wanawake na washichana wa Kipalestina.
Riyadh al Ashqar, msemaji wa vyombo vya habari wa kituo cha mteka wa Palestina amenukuliwa na shirika la habari la Qudsuna akisema leo Jumatatu kwamba, wanajeshi wa utawala katili wa Kizayuni wameshadidisha kuwateka nyara wanawake na wasichana wa Kipalestina na kwamba wasichana na wanawake 215 wameshatiwa mbaroni na wanajeshi wa Israel katika kipindi hiki cha miezi minane na nusu ya tangu ilipoanza Intifadha ya Quds mwezi Oktoba 2015. Tangu wakati huo maeneo mbalimbali ya ardhi za Palestina yamekuwa yakishuhudia malalimko ya kila namna ya Wapalestina wanaopinga siasa za kikatili za utawala wa wa Kizayuni wa Israel. Wapalestina hao wanalalamikia pia njama za Wazayuni za kuvuruga muundo wa watu na wa kijiografia wa ardhi za Palestina pamoja na njama za kuubomoa msikiti wa al Aqsa, Kibla cha Kwanza cha Waislamu. Jinai za utawala wa Kizayuni ndizo zilizopelekea kuanza Intifadha ya Quds mwaka jana na kuendelea hadi hivi sasa. Habari nyingine zinasema kuwa, leo Jumatatu, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wamewakamata vibarua 27 wa Kipalestina kwa madai ya kuingia mjini Tel Aviv bila ya kibali. Kila leo wanajeshi wa utawala kandamizi wa Kizayuni unawateka nyara Wapalestina kwa madai tofauti.