Wabahrain waandamana kulaani safari ya Rais wa Israel nchini kwao
Maandamano makubwa ya kupinga safari ya Rais Isaac Herzog wa utawala haramu wa Israel yamefanyika katika mji mkuu wa Bahrain, Manama.
Waandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu walisikika wakipiga nara dhidi ya utawala haramu wa Israel na kutangaza kuliunga mkono taifa madhulumu la Palestiina.
Kadhalika waandamanaji hao mbali na kulaani jinai za Israel huko Palestina wamechoma moto picha za Rais Isaac Herzog wa wa utawala haramu wa Israel na kulaani vikali kitendo cha utawala wa Manama cha kumkaribisha Rais huo katika ardhi ya Bahrain.
Waandamanaji hao ambao kimsingi wameandamana kupinga safari ya rais wa utawala ghasibu wa Israel nchini bahrain wamelaani vikali hatua ya utawala wa Bahrain ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.
Bahrain ilitia saini makubaliano ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel chini ya usimamizi wa Marekani katika Ikulu ya White House mnamo Septemba 2020. Tangu wakati huo, tawala za Manama na Tel Aviv zimekuwa zikijaribu kuimarisha uhusiano huku Wapalestina na wafuasi wao wa kieneo na kimataifa wakiutaja uhusiano huo kuwa ni usaliti kwa harakati ya kupigania ukombozi wa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Israel.
Wanaoikosia safari ya Herzog nchini Bahrain ambaye tayari amekamilisha safari yake nchini humo na kuwasili huko Imarati kama kituo chake cha pili wanasema kuwa, hatua inayolenga kupuuza ukatili na vitendo vya kigaidi vya utawala ghasibu wa Israel.