-
Qatar: Inabidi UN itoe azimio la kuilazimisha Israel iheshimu usimamishaji vita Ghaza
Jan 18, 2025 03:14Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amesisitiza kuwa jumuiya ya kimataifa inapaswa kutoa msaada unaohitajika wa kuzisaidia familia zilizoathirika katika mashambulizi ya kikatili ya Israel huko Ghaza na kuhakikisha kunatolewa azimio ambalo litaulazimisha utawala wa Kizayuni kuheshimu usimamishaji vita.
-
Guterres aitaka Israel kusitisha ukiukaji wa azimio nambari 1701 kusini mwa Lebanon
Jan 17, 2025 23:11Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameitaka Israel ikomeshe kukalia kwa mabavu ardhi ya Lebanon na kufanya operesheni za kijeshi ndani ya nchi hiyo, akisisitiza kuwa vitendo hivi vinakiuka azimio nambari 1701 la Baraza la Usalama.
-
Israel imewauwa shahidi Wapalestina zaidi ya 100 huko Gaza licha ya tangazo la usitishaji vita
Jan 17, 2025 10:27Idara ya Ulinzi wa Raia ya Gaza imetangaza leo Ijumaa kuwa Wapalestina wasiopungua 101, wakiwemo watoto 27 na wanawake 31, wameuawa shahidi katika mashambulizi ya Israel tangu kutangazwa makubaliano ya kusitisha mapigano juzi Jumatano.
-
HAMAS: Israel imeshambulia kwa mabomu mahali alipokuwa anashikiliwa mateka mmoja wa Israel
Jan 16, 2025 23:49Abu Ubaydah, msemaji wa Brigedi za Izzuddin Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel jana Alkhamisi lilishambuliwa kwa makusudi eneo ambalo mateka mmoja wa kike wa Israel alikuwa akishikiliwa kwenye Ukanda wa Ghaza.
-
Vikwazo; Fimbo ya Magharibi katika sera ya kigeni
Jan 16, 2025 23:25Wakati Marekani na nchi za Ulaya zimekuwa na nafasi kubwa katika kuwawekea mashinikizo ya kiuchumi watu wa Syria kwa kutumia vikwazo vya kikatili, sasa baada ya kuanguka utawala wa Bashar al-Assad na kushika madaraka kundi la Hay'at Tahrir al-Sham, kuna minong'ono kwamba nchi hizo zina nia ya kupunguza vikwazo dhidi ya nchi hiyo.
-
Kuchunguzwa matokeo ya usitishaji vita Ukanda wa Gaza
Jan 16, 2025 09:50Baada ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) kutangaza rasmi kukubali usitishaji vita na kuanza mchakato wa kuhitimisha vita katika ukanda huo, hapana shaka kuwa masuuala ya kimedani na kisiasa katika eneo hilo yataathiriwa na tukio hilo.
-
Gaza imeshinda: Watumiaji wa mitandao ya kijamii wazungumzia usitishaji mapigano Gaza
Jan 16, 2025 07:47Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamezungumzia habari ya makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Hamas na Israel katika Ukanda wa Gaza kwa hisia mchanganyiko za furaha na matumaini ya mustakbali mwema.
-
Israel yasalimu amri baada ya kushindwa kuiangamiza HAMAS
Jan 16, 2025 04:07Baada ya mapigano ya miezi 15 huko Ghaza hatimaye utawala wa Kizayuni wa Israel umelazimika kusalimu amri na kukubali makubaliano ya kusitisha mapigano bila ya kufanikiwa kuiangamiza Hamas wala kokomboa mateka wa Kizayuni.
-
Hamas: Makubaliano ya kusitisha vita ni matunda na Muqawama wa miezi 15 wa wananchi wa Ghaza
Jan 16, 2025 04:03Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imesema kuwa, kulazimika utawala wa Kizayuni kukubali kusimamisha vita na kukomesha mauaji yake ya kimbari dhidi ya wananchi wa Ghaza, ni matunda ya Muqawama na kusimama imara wananchi wa ukanda huo kwa zaidi ya miezi 15.
-
Israel imeshaua Wapalestina 40 Ghaza tangu baada ya kutangazwa makubaliano ya kusitisha vita
Jan 16, 2025 00:07Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limeendeleza mashambulio katika Ukanda wa Ghaza licha ya kutangazwa makubaliano ya kusitisha vita kati ya utawala huo ghasibu na Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS. Hadi wakati huu, Wapalestina wasiopungua 40 wameshauliwa shahidi na jeshi hilo.