-
Israel imeua shahidi zaidi ya Wapalestina 50 huko Ghaza katika siku moja
Jan 14, 2025 05:44Idara ya Ulinzi ya Raia ya Gaza imetangaza kuwa zaidi ya Wapalestina 50 wameuawa shahidi kwenye mashambulizi ya anga ya Israel katika muda wa saa 24 zilizopita kwenye Ukanda wa Ghaza, ambao unaendelea kuteseka kwa janga la kibinadamu lililosababishwa na mauaji ya kimbari ya utawala katili wa Israel.
-
Wanajeshi wa Israel wakiri kufanya uhalifu wa kivita huko Gaza
Jan 14, 2025 04:15Shirika la habari la Associated Press limeripoti ushuhuda kutoka kwa wanajeshi wa Israel ambao wamekiri kufanya uhalifu wa kivita, kuwalenga watu wasio na ulinzi, na kuharibu na kupora nyumba ambazo hazikuwa tishio wakati wa ushiriki wao katika uvamizi unaoendelea kwenye Ukanda wa Gaza.
-
Chuo Kikuu cha al-Azhar chalaani kimya cha walimwengu kwa jinai za Israel huko Gaza
Jan 13, 2025 23:44Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri kimelaani vikali ukimya wa jamii ya kimataifa na kutojali mgogoro wa kibinadamu ulioibuliwa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
-
Wapalestina wengine 19 wauawa shahidi
Jan 13, 2025 23:40Wapalestina wengine 19 wameuawa shahidi katika muendelezo wa jinai za utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
-
Wanajeshi 3 wa Israel waangamizwa kaskazini mwa Ukanda wa Gaza
Jan 13, 2025 07:41Wanajeshi 3 wa Kizayuni wameangamizwa katika shambulizi la kuvizia la wanamuqawama dhidi ya Wazayuni kaskazini mwa Gaza.
-
UNICEF: Zaidi ya watoto milioni moja wa Gaza wanasumbuliwa na tatizo la afya ya akili
Jan 13, 2025 07:26Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Watoto (UNICEF) umeonya kuwa karibu watoto wote milioni 1.1 katika Ukanda wa Gaza wanakabiliwa na mgogoro wa afya ya akili na wanahitaji msaada wa kisaikolojia, huku utawala wa Israel ukiendeleza vita vya kikatili dhidi ya wakazi wa eneo hilo linalozingirwa.
-
Namna vipimo vya undumilakuwili vya Magharibi vinavyochangia kuendelea jinai za Wazayuni dhidi ya Wapalestina wa Ghaza
Jan 13, 2025 03:58Francesca Albanese, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu amesema, Israel inavitumia vipimo vya undumilakuwili vya nchi za Magharibi kuendeleza jinai na uhalifu wake katika Ukanda wa Ghaza.
-
Makamanda wengi wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel wameangamizwa Ghaza
Jan 13, 2025 00:00Brigedia Jenerali mstaafu wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel amefichua kuwa asilimia 80 ya makamanda wa Brigedi ya Givati wameuawa au kujeruhiwa katika vita dhidi ya Ukanda wa Ghaza.
-
UN: Taswira za viwiliwili, hali ya njaa na uharibifu inayoonekana Ghaza ni ya "kutisha"
Jan 12, 2025 23:57Mkuu wa mawasiliano ya dharura wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP ameitaja hali ya mauaji, njaa na uharibifu unaosababishwa na uvamizi wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza kuwa ni ya "kutisha".
-
Gazeti la Kiebrania la Haaretz: Israel imeidhinisha mpango wa kuondoa askari wake Ukanda wa Ghaza
Jan 12, 2025 23:56Gazeti la Kiebrania la Haaretz limeripoti kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel umeidhinisha mipango ya kuwaondoa wanajeshi katika Ukanda wa Ghaza, baada ya hatua zilizopigwa katika mazungumzo ya kubadilishana mateka na harakati ya Hamas.