-
Netanyahu ashikilia msimamo wake wa kupinga kuundwa nchi huru ya Palestina
Apr 05, 2024 23:09Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu amerudia tena msimamo wake wa kupinga katakata kuundwa nchi huru ya Palestina alipokutana na ujumbe wa Marekani wa wabunge wa chama cha Republican.
-
OCHA: Tangu Oktoba 7, Israel imefanya mashambulio zaidi ya 700 Ukingo wa Magharibi na kuua watu 428
Apr 05, 2024 23:08Ukiwa unakaribia kutimia mwezi wa sita tangu utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ulipoanzisha vita vya kinyama na mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza, Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, katika kipindi hicho, zaidi ya mashambulizi 700 yamefanywa na utawala huo ghasibu dhidi ya Wapalestina wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan unaokaliwa kwa mabavu ikiwemo Baitul Muqaddas Mashariki.
-
Kiongozi wa Ansarullah: Tumeshambulia meli 90 zinazohusiana na Israel katika Bahari ya Sham
Apr 05, 2024 10:22Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen Sayyid Abdul Malik Badruddin al-Houthi amesema, wapiganaji wa harakati hiyo wameshambulia meli 90 za Israel au zile zinazoelekea bandari za utawala huo wa Kizayuni katika eneo la Bahari ya Sham mbali na kuongeza na kupanua wigo wa mashambulio ya ndege zisizo na rubani katika maeneo mengine.
-
Siku ya Kimataifa ya Quds; Siku ya mwamko wa Ulimwengu wa Kiislamu
Apr 05, 2024 04:22Leo Ijumaa tarehe 5 mwezi Aprili inayosadifiana na tarehe 25 Ramadhani 1445 hijria shamsia ni Siku ya Kimataifa ya Quds.
-
Wanajeshi wa Israel wazuiliwa kwenda livu ya nyumbani kwa tahadhari na hofu ya shambulio la Iran
Apr 04, 2024 22:53Jeshi la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel limesitisha livu ya nyumbani kwa wanajeshi wake kutokana na kuwepo hofu inayoongezeka ya utawala huo kuandamwa na shambulio la kulipiza kisasi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Iran kufuatia shambulio la kigaidi ulilofanya wiki hii kwenye ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria.
-
Yemen: Siku ya Kimataifa ya Quds imeibakisha hai kadhia ya Palestina
Apr 04, 2024 08:01Katibu wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amesema kuwa, Siku ya Kimataifa ya Quds imeyabakisha hai mapambano ya ukombozi wa Palestina.
-
Siku ya Quds na kufichuka sura halisi ya utawala wa mauaji ya kimbari wa Israel
Apr 04, 2024 04:51Siku ya Quds mwaka huu 2024 imewadia huku utawala wa Kizayuni wa Israel ukiwa umekwama kwenye kinamasi cha Gaza licha ya mauaji ya kimbari unayoendelea kufanya katika eneo hilo la Palestina.
-
Hassan Nasrullah: Kimbunga cha al-Aqsa kimemsukuma adui Mzayuni kwenye ukingo wa shimo la mauti
Apr 04, 2024 03:22Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu ni tofauti na miaka iliyopita, na kwamba operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa imemweka adui Mzayuni kwenye ukingo wa shimo la mauti.
-
Kufungwa kituo cha televisheni cha Al Jazeera Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel)
Apr 04, 2024 01:15Radimali ya jinai za Israel dhidi ya watu wa Gaza katika vyombo vya habari vya dunia na wimbi la upinzani na lawama za kimataifa kuhusu jinai hizo zimeufanya utawala wa Kizayuni kufunga mara moja kituo cha Televisheni ya Al-Jazeera katika Ukanda wa Gaza kutokana na jinsi inavyoakisi habari za mauaji ya kimbari ya utawala huo katika vita hivyo.
-
VIDEO: Muqawama wa Iraq: Tumeshambulia Haifa kulipiza kisasi cha jinai za Wazayuni Ghaza
Apr 03, 2024 03:38Makukndi ya Muqawa wa Kiislamu ya Iraq yametangaza kuwa yameshambulia kambi ya jeshi la anga ya Tel Nof ya utawala wa Kizayuni kwenye mji wa Haifa ili kulipiza kisasi cha jinai zinazofanywa na Israel katika Ukanda wa Ghaza.