Sep 12, 2023 02:26 UTC
  • Kuongezeka mpasuko katika G20

Wakati Marekani inajaribu kueneza fikra kwamba kundi la G20 ni mojawapo ya mashirika ya kimataifa yenye mpangilio bora zaidi ambako Washington inaweza kutumia ushawishi wake kuongoza shughuli zake, malengo na mipango yake, lakini mkutano wa G20 huko nchini India na upinzani wa China dhidi ya kufanyika mkutano wa 2026 nchini Marekani vinaonyesha kuongezeka kwa tofauti na mpasuko katika G20.

Kutohudhuria viongozi wa Russia na Uchina katika mkutano wa G20 nchini India kunaonyesha kuwa, kutokana na kuhamia nguvu ya kimataifa upande wa Mashariki, nchi kama Marekani hazina tena uwezo unaohitajika wa kuwa na ushawishi kwenye matukio ya kimataifa na kuyaendesha kwa mujibu wa matakwa na maoni yao. Daniel Kowalik, mtaalamu wa masuala ya kimataifa, anasema: "Inaonekana Marekani bado haiamini kwamba myororo wa kuhama madaraka na nguvu kutoka Magharibi hadi Mashariki unaelekea kukamilika, na miundo na jumuiya ambazo zilianzishwa na madola ya Magharibi, hasa Marekani, ikiwa ni pamoja na kundi linalojulikana kama G20, ili kupeleka mbele malengo yao, zimepoteza uwezo na ufanisi wao. Ukweli huu unaonekana wazi kabisa kutokana na upinzani wa wanachama wake muhimu kwa maamuzi na mitazamo ya Marekani." 

Raisi wa China, Xi Jinping na mwenzake wa Marekani, Joe Biden

Katika muktadha huo, pingamizi la China dhidi ya kuandaliwa mkutano wa G20, 2026 huko Marekani pia limeungwa mkono na kuidhinishwa na Russia. Taarifa ya G20 inaonyesha wazi kuwa, Marekani imejaribu kutumia fursa ya mkutano huo kulaani Russia kutokana na vita vya Ukraine. Ingawa taarifa iliyochapishwa katika mkutano wa mwaka jana wa viongozi wa G20 huko Bali, Indonesia, ilikuwa dhidi ya Russia kikamilifu, lakini taarifa ya mkutano wa kilele wa New Delhi imekuwa na lugha laini zaidi kuhusiana na Russia, kwa kuzingatia uhusiano wa kimkakati baina ya New Delhi na Moscow, japokuwa lugha iliyotumiwa ilikuwa dhidi ya Moscow kwa maslahi ya serikali ya Kiev. Wakati huo huo, angalau nchi wanachama wa G20 ambazo zinafuata njia ya mantiki, zingeweza kutaja baadhi ya nukta muhimu katika taarifa ya mwisho kuhusu sababu za kutokea vita huko Ukraine na sera za hujuma na uvamizi za Marekani katika mfumo wa NATO dhidi ya Mashariki, na vilevile kuongezeka kwa vitisho vya shirika hilo la kijeshi. Hi Sing Tso, mtaalamu wa masuala ya kimataifa anasema: "Marekani inajaribu kulazimisha sera na malengo yake katika taarifa za mwisho za mikutano kama wa G20, wakati njia ya haki ni kuashiria sera za uchokozi za Marekani na NATO dhidi ya Mashariki na njama zake za kuibana Russia katika mipaka yake. Kupanuka jiografia ya NATO upande wa Mashariki ni tishio kubwa la usalama kwa nchi kama Russia na hata Uchina."

Mkutano wa G20, India

Vyovyote vile, ingawa G20 ni shirika la kimataifa linalojumuisha nchi 19 pamoja na Umoja wa Ulaya, ambalo linafanya kazi kushughulikia masuala makubwa yanayohusiana na uchumi wa dunia, kama vile utulivu katika masoko ya kifedha ya kimataifa, kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, na maendeleo endelevu, lakini Marekani imepindisha malengo na sheria za kundi hilo, kama inavyofanya katika mashirika mengine ya kimataifa, na imejaribu kulifanya jukwaa la kustawisha malengo na mipango yake miovu. Kwa sababu hii, mashirika ya kikanda na kimataifa ambayo Marekani ni mwanachama wake hayasaidii lolote katika kutatua matatizo ya kimataifa, bali zaidi ni kwamba, tofauti na mipasuko kati ya wanachama wake inaongezeka zaidi. Kwa kadiri kwamba, nchi za Mashariki, zikiwemo China na Russia, zinapiga hatua kuelekea upande wa kupanua mashirika ya kimataifa kama BRICS, ambayo yanaweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kutokana na kutokuwepo Marekani ndani ya makundi hayo. 

Tags