Dec 04, 2023 02:59 UTC
  • Waislamu Marekani waapa

Waislamu katika majimbo muhimu ya Marekani wamezindua kampeni ya #AbandonBiden kutokana na kukataa kwa rais huyo wa Merekani kutoa wito wa kusitishwa mashambulizi ya kinyama ya Israel huko Ukanda wa Gaza.

Viongozi wa Kiislamu wa Marekani katika majimbo kadhaa muhimu wameahidi kuzikusanya pamoja jumuiya zao dhidi ya azma ya Rais Joe Biden ya kuchaguliwa tena kutokana na uungaji mkono wake mkubwa kwa vita na mashambulizi ya Israel dhidi ya watu wa Gaza.

Kampeni ya #AbandonBiden ilianza wakati Wamarekani Waislamu wa Minnesota walipomtaka Biden atoe wito wa kusitisha mapigano ifikapo Oktoba 31, na kuenea hadi huko Michigan, Arizona, Wisconsin, Pennsylvania na Florida.

kundi hilo limekkiambia chombo cha habari cha Axios kwamba: "Kampeni hii ya #AbandonBiden 2024 imeandaliwa kwa kuzingatia uchaguzi ujao wa rais wa 2024 na uamuzi wa kutomuunga mkono Rais Biden kwa sababu ya kutokuwa kwake tayari kutoa wito wa kusitishwa mapigano na kuwalinda raia wasio na hatia huko Palestina na Israel."

Upinzani wa idadi kubwa ya Waislamu na Wamarekani Waarabu dhidi ya Biden unaweza kutoa changamoto kwa wajumbe wa kamati maalumu ya uchaguzi nchini Marekani maarufu kama Electoral College katika uchaguzi ujao wa rais.

Rais wa Marekani na makamu wake huchaguliwa na kundi la "wapiga kura" (Electoral College) ambao mara nyingi huchaguliwa na vyama vya kisiasa katika majimbo ya nchi hiyo.

Maafisa wa Marekani wameendelea kupuuzua mashinikizo ya walimwengu wanaotaka kusitishwa mashambulizi ya kikatili na mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel dhidi ya raia wa Palestina.

Wapalestina karibu elfu 16 wameuawa hadi sasa katika mashambulizi hayo. 

Tags