Apr 11, 2024 07:53 UTC
  • Rais wa Marekani aona

Rais Joe Biden wa Marekani amepongeza upanuzi zaidi wa shirika la kijeshi la NATO kuelekea mipaka ya Russia, huku akimshutumu mpinzani wake wa Republican Donald Trump kwamba amedhoofisha umoja wa kambi hiyo ya kijeshi inayoongozwa na Marekani.

Kwa miaka kadhaa, Russia imeelezea wasiwasi wake juu ya kunyemelewa na uvamizi unaoenea wa NATO, na kuzielezea sera za shirika hilo kama tishio halisi lililopo.
 
Katika mahojiano na shirika la utangazaji la lugha ya Kihispania Univision ambayo yalirushwa hewani siku ya Jumanne, Biden alipongeza na kulitaja kama mafanikio makubwa ongezeko la wanachama wa NATO la hivi karibuni lililojumuisha nchi za Finland na Sweden kwenye safu ya kambi hiyo ya kijeshi huku kukiwepo mzozo wa kivita wa Ukraine.

Rais wa Marekani ameeleza katika mahojiano hayo: "tumefanya jambo ambalo nimejivunia sana. Nimejihusisha na NATO katika muda wote wa majukumu yangu. Tuliweza kupanua NATO, na tuna masafa ya umbali wa maili 2,000 kwa sababu una mataifa mawili ya Nordic ambayo yamejiunga na NATO. Una safu nzima ya nchi za NATO kwenye mpaka wa Russia".

 
Rais Vladimir Putin wa Russia alishaonya tokea miongo karibu miwili nyuma kwamba sera za NATO zinadhoofisha usalama wa taifa la Russia lakini "mstari mwekundu" halisi wa Moscow utakuwa jaribio la kuhamisha vikosi vya umoja huo na kuvipeleka Ukraine.
 
Mnamo mwezi Februrai 2022, Putin alisema, mzozo wa Ukraine ni wa kupigania "kubaki" kwa Moscow na ni "suala la kufa na kupona," wakati kwa Magharibi ni suala la "kuboresha misimamo yake ya kimbinu".../

Tags