Jul 23, 2016 06:57 UTC
  • Radiamali ya Umoja wa Mataifa kwa shambulizi la Munich, Ujerumani

Umoja wa Mataifa umelaani shambulio la ufyatuaji risasi lililotokea katika jumba la biashara katika mji wa Munich nchini Ujerumani.

Farhan Haq Msemaji wa Ban Ki-moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani ufyatuaji risasi wa umwagaji damu uliotokea katika jumba la biashara la Munich Ujerumani na kusisitiza kutiwa mbaroni na kuhukumiwa wahusika wa shambulio hilo. 

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema lengo la kutekelezwa shambulio hilo ni kuua raia na kuongeza kuwa Umoja wa Mataifa uko pamoja na wananchi wa Ujerumani kufuatia kujiri shambulio hilo la kuhuzunisha lililosababisha vifo vya raia.

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq 

Wakati huo huo polisi wa mji wa Munich wametangaza kuwa hadi sasa hawajafahamu watu waliotekeleza shambulio hilo walikuwa na lengo gani. Polisi wamesema kuwa wanaendelea kufanya uchunguzi kuhusu tukio hilo. Watu 11 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ufyatuaji risasi uliotekelezwa jana alasiri katika jumba la biashara huko Munich Ujerumani. Hii ni katika hali ambayo usafiri wa metro katika mji wa Munich umesimamishwa huku hali ya hatari ikitangazwa katika hospitali zote za mji huo. 

Tags