Sullivan: Enzi ya ukuu wa Marekani imekwisha
Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Ikulu ya Rais wa Marekani, White House, amekiri kwamba: Zama za Marekani kuwa juu zaidi ya nchi nyingine zimekwisha na kuyoyoma.
Akizungumza katika mahojiano na gazeti la Marekani la The New York Times, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Ikulu ya White House, Jake Sullivan, ameashiria mwisho wa mfumo wa utawa wa Marekani duniani na kusema: “Enzi ya baada ya Vita Baridi imekwisha; Zama za utawala wa Marekani kuanzia miaka ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000 zimeyoyoma. Kabla ya utawala wa Biden kuingia madarakani, enzi ya ukuu wa Marekani ilikuwa imekwisha."
Sullivan amezungumzia pia vita vya Gaza na amehalalisha mashambulizi yanayofanywa na utawala wa Israel dhidi ya hospitali, misikiti makanisa na maeneo mengine ya raia huko Gaza, akidai kuwa Hamas kuwa inatumia shule, misikiti na hospitali kwa madhumuni ya kijeshi.
Hii ni pamoja na ukweli kwamba madai hayo yamepingwa na Umoja wa Mataifa, nchi za Ulaya na hata baadhi ya maafisa wa Israel na Marekani.
Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa, zaidi ya asilimia 70 ya mashahidi waliouawa na Israel huko Gaza ni wanawake na watoto.