Kwa nini kunaibuka ufa baina ya Marekani na Ulaya?
https://parstoday.ir/sw/news/world-i135334-kwa_nini_kunaibuka_ufa_baina_ya_marekani_na_ulaya
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amekosoa mwelekeo wa sera za kigeni za Marekani hivi sasa na kusema hivi sasa Marekani imeanza hatua kwa hatua kujiweka mbali na waitifaki wake sambamba na kukiuka sheria za kimataifa.
(last modified 2026-02-05T12:50:29+00:00 )
Jan 11, 2026 02:29 UTC
  • Kwa nini kunaibuka ufa baina ya Marekani na Ulaya?
    Kwa nini kunaibuka ufa baina ya Marekani na Ulaya?

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amekosoa mwelekeo wa sera za kigeni za Marekani hivi sasa na kusema hivi sasa Marekani imeanza hatua kwa hatua kujiweka mbali na waitifaki wake sambamba na kukiuka sheria za kimataifa.

Macron katika ukosoaji wake huo kuhusu sera mpya za kigeni za Marekani amesema: "Marekani ni dola lenye nguvu lakini ambalo sasa hatua kwa hatua linajitenga na baadhi ya waitifaki wake na inakiuka sheria za kimataifa ambazo yenyewe imekuwa ikitaka zizingatiwe." Macron  amesema sera hizo zimepelekea taasisi za kimataifa zidhoofike zaidi.

Watawala wa nchi za Ulaya sasa wanazungumza kuhusu kujitenga na Marekani katika hali ambayo kwa miongo kadhaa wamekuwa washirika wa Marekani. Hatahivyo katika miaka ya hivi karibuni  hasa wakati wa urais wa Trump, ufa baina ya Marekani na Ulaya umezidi kupanuka. Kimsingi, Marekani chini ya utawala wa Trump inafuatilia sera za upande mmoja kwa msingi wa maslahi ya Marekani bila kujali maslahi ya waitifaki wake jambo ambalo ni kinyume cha sera Ulaya za ushirikiano wa pande kadhaa.

Trump alianza utawala wake kwa nara ya 'Marekani Kwanza' na amekuwa akichukua maamuzu ya upande mmoja bila kushauriana na waitifaki hasa katika muungano wa kijeshi wa NATO. Mfano wa wazi wa hivi karibuni ni uamuzi wake wa kuishambulia Venezuela na kumteka nyara rais wa nchi hiyo Nicholas Maduro na mkewe na pia kujiondoa Marekani katika taasisi zaidi ya 60 za kimataifa na Umoja wa Mataifa.

Kimsingi katika duru ya pili ya urais wake, ufa baina ya Marekani na Ulaya umezidi kupanuka katika masuala mbali mbali  ya kisiasa, kiuchumi na kiusalama. Mgawanyiko baina ya Marekani na Ulaya ulishadidi zaidi wakati Trump alipoongeza ushuru kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka Ulaya. Katika uga wa kiusalama, misimamo ya Trump imepelekea nchi za Ulaya zianze kutafakari kuhusu kuanzisha muungano mpya wa kijeshi kutokana na mgawanyiko uliopo katika NATO.

Katika uga wa kisiasa pia, kuongezeka harakati ya vyama vya kisiasa vya wazungu wenye misimamo mikali Ulaya, kuibuka mienendo ya kutaka kujitenga baadhi ya nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya, hatari ya hujuma za kigaidi na pia ongezeko la wahajiri wa kigeni sambamba na ongezeko la bajeti ya kijeshi kutokanana na vita vya Ukraine ni mambo ambayo yamepelekea bara Ulaya kukumbwa na hali ngumu hivi sasa. Hali imekuwa mbaya kiasi kwamba baadhi ya nchi za Umoja wa Ulaya zinataka kujitenga na umoja huo.

Katika upande mwingine, kushadidi hitilafu katika sera  za kigeni baina ya Marekani na Umoja wa Ulaya kumepelekea nchi za Ulaya zihisi kuwa si waitifaki wa Marekani.  Rais Macron wa Ufaransa amekiri mara kadhaa kuhusu hitilafu na mgawanyiko unaozidi kuongezeka baina ya Marekani na nchi za Ulaya. Kansela wa Ujerumani hivi karibuni katika mahojiano na gazeti la Franfuter Algamaine Zeittung alitangaza rasmi kuwa: "Katika hali ya hivi sasa, nchi za Ulaya, hata kama zinataka, haziwezi kuwa na ushawishi mkubwa katika eneo la Asia Magharibi." Ameashiria migogoro mikubwa   ambayo sasa inazishughulia nchi za Ulaya.  Kwa mfano katika kadhia ya eneo la Greenland la Denmark, Rais Trump wa Marekani ametoa matamshi ya kuwa anataka kulipora eneo hilo liwe ardhi ya Marekani na hivyo kuibua taharuki kote  Ulaya.

Rais Donald Trump wa Marekani amedai kuwa kuliteka eneo la Greenland ni jambo la dharura kwa ajili ya kulinda usalama wa taifa wa Marekani na kusema: Kunyakua Greenland yumkini kukafanyika kwa njia za amani au kwa kutumia mabavu. 
Viongozi wa Ulaya wamekosoa vikali matamshi hayo ya Trump. Viongozi wa Italia, Poland, Hispania na Uingereza, Ufaransa na Ujerumani wametoa taarifa na kusema kisiwa cha Greenland ni cha watu wa eneo hilo. Greenland ina eneo la kimkakati la kijiografia na rasilimali nyingi za madini. Kisiwa hicho cha Denmark ndicho njia fupi zaidi kati ya Ulaya na Amerika Kaskazini.

Ingawa  bara Ulaya lingali muitifaki mkubwa zaidi wa Marekani, lakini kuendelea sera za hivi sasa za Trump kumepelekea wakuu wa nchi za Ulaya kutangaza bayana misimamo yao ya kumpinga wazi wazi mtawalahuyo wa Marekani. Hivi sasa nchi za Ulaya zinatafakari kwa kuna kuhusu kuimarisha uhusiano wa kimkakati na nchi zingine duniani badala ya kutegemea muungano wa kijeshi wa NATO kwani zinahisi haziwezi kujihesabu tena kuwa waitifaki wa Marekani.