Waziri wa Elimu Ufaransa akosoa marufuku ya vazi la burqini
https://parstoday.ir/sw/news/world-i14009-waziri_wa_elimu_ufaransa_akosoa_marufuku_ya_vazi_la_burqini
Waziri wa Elimu nchini Ufaransa, Najat Vallaud-Belkacem amekosoa marufuku ya vazi la stara la kuogelea linalovaliwa na wanawake wa Kiislamu linalofahamika kwa jina la 'Burqini' ambalo lilikatazwa hivi karibuni na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Manuel Valls.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 26, 2016 11:37 UTC
  • Waziri wa Elimu Ufaransa akosoa marufuku ya vazi la burqini

Waziri wa Elimu nchini Ufaransa, Najat Vallaud-Belkacem amekosoa marufuku ya vazi la stara la kuogelea linalovaliwa na wanawake wa Kiislamu linalofahamika kwa jina la 'Burqini' ambalo lilikatazwa hivi karibuni na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Manuel Valls.

 Najat Vallaud-Belkacem amesema kuwa, baadhi ya nukta zilizomo katika marufuku hiyo zinawakandamiza wanawake katika hali ambayo serikali haitakiwi kuwalazimisha wananchi kuachana na dini zao.

Mwanamke wa Kiislamu akiwa amevalia vazi la stara wakati wa kuogelea

Ameongeza kuwa hatua ya serikali ya nchi hiyo ya kupiga marufuku vazi hilo la burqini kwa wanawake Waislamu ni kukanyaga uhuru wa mtu binafsi.

Waziri Mkuu wa Ufaransa Manuel Valls amepiga marufuku vazi hilo akidai kuwa, marufuku hiyo ni kwa ajili ya kulinda utukufu wa wanawake. Valls alisema kuwa, vazi hilo na mavazi mengine ya stara ikiwemo burqa, yanamfanya mwanamke kuwa mtumwa na kwamba serikali inapinga suala hilo.

Katika sehemu nyingine ya matamshi makali ya Waziri Mkuu wa Ufaransa, Manuel Valls alidai kuwa vazi la Wanawake wa Kiislamu la burqini ni alama ya misimamo mikali.

Vazi la kuogelea la burqini kwa ajili ya mwanamke wa Kiislamu 

Awali baadhi ya mameya wa miji kadhaa ya Ufaransa walipiga marufuku uvaaji wa mavazi ya stara la Kiislamu katika pwani za nchi hiyo, suala ambalo liliungwa pia mkono na serikali.