Trump: Marekani ilifanya makosa kuzivamia nchi za Iraq na Afghanistan
https://parstoday.ir/sw/news/world-i23572-trump_marekani_ilifanya_makosa_kuzivamia_nchi_za_iraq_na_afghanistan
Rais mteule wa Marekani amesema kuwa nchi hiyo ilifanya makosa kuzivamia nchi za Iraq na Afghanistan.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 16, 2017 03:03 UTC
  • Trump: Marekani ilifanya makosa kuzivamia nchi za Iraq na Afghanistan

Rais mteule wa Marekani amesema kuwa nchi hiyo ilifanya makosa kuzivamia nchi za Iraq na Afghanistan.

Katika mahojiano yake yaliyochapishwa leo na gazeti la Times la Uingereza, Donald Trump amekosoa siasa za nje za Marekani na kusema: Uvamizi wa Iraq na Afghanistan ni miongoni mwa maamuzi mbaya zaidi katika historia ya Marekani. 

Askari wa Marekani katika ardhi ya Iraq

Trump pia amepongeza uamuzi wa Waingereza wa kuijiondoa kwenye Umoja wa Ulaya na kutabiri kuwa, nchi nyingine za Ulaya pia zitajiondoa katika umoja huo. Amesema uamuzi huo ulikuwa hatua kubwa na ya busara na kuongeza kuwa Waingereza wanataka kurejeshewa utambulisho wao.

Image Caption

Katika sehemu nyingine ya mahojiano hayo rais mteule wa Marekani amekosoa mapambano ya Russia dhidi ya ugaidi nchini Syria bila hata ya kuashiria nchi zilizoanzisha mgogoro wa Syria na kuwapa misaasa ya kifedha na kisiasa magaidi hao.

Donald Trump pia ameingilia masuala ya ndani ya Syria kwa kutoa wito wa kutengwa maeneo eti ya amani nchini humo. 

Magaidi wa kundi la Daesh wanaoungwa mkono na Marekani huko Syia

Trump ametoa matamshi hayo kuhusu Syria na kujisahaulisha kuwa Marekani ni miongoni mwa waanzilishi na wasaidizi wakubwa wa makundi ya kigaidi katika nchi za Syria na Iraq na imekuwa na nafasi kubwa katika kuanzisha na kudumisha mgogoro wa sasa katika nchi hizo.