Mar 31, 2017 07:25 UTC
  • Kamanda wa jeshi la Saudia apigwa mayai Uingereza

Ahmed al-Asiri, mshauri wa Wizara ya Ulinzi ya Saudia na msemaji wa muungano vamizi wa Saudia dhidi ya Yemen, ameshambuliwa na waandamanaji wanaopinga hujuma za utawala wa Aal-Saud nchini Yemen na kupigwa mayai mabovu.

Awali waandamanaji hao walijitahidi sana kuzuia kufika Ahmed al-Asiri katika kikao cha 'Baraza la Mahusiano ya Nje la Ulaya' kilichokuwa kimeitishwa kwa ajili ya kuchunguza mgogoro wa Yemen. Katika maandamano hayo, Sam Watson mwanaharakati wa kupigania amani nchini Uingereza, alisisitizia umuhimu wa kutiwa mbaroni mshauri huyo wa Wizara ya Ulinzi ya Saudia na msemaji wa muungano vamizi wa Saudia nchini Yemen kutokana na jinai za nchi yake dhidi ya taifa hilo jirani la Kiarabu.

Moja ya jinai za kutisha za Saudia nchini Yemen 

Ahmed al-Asir alienda mjini London, Uingereza kwa ajili ya kuhutubia Baraza la Mahusiano ya Nje la Ulaya.' Hata hivyo wakati anaingia katika kikao hicho alijikuta akichafuliwa nguo zake kwa kupigwa mayai mabovu mwilini. Hayo yanajiri katika hali ambayo katika nchi mbalimbali za Magharibi, kumekuwa kukishuhudiwa maandamano ya wanaharakati, kulaani jinai za Saudi Arabia dhidi ya raia wasio na ulinzi wa Yemen.

Ahmed al-Asiri, mshauri wa Wizara ya Ulinzi ya Saudia na msemaji wa muungano vamizi wa Saudia nchini Yemen

Saudia kwa kushirikiana na Marekani, Uingereza, utawala haramu wa Kizayuni wa Israel na baadhi ya nchi za Kiarabu ilianzisha mashambulizi ya kila upande nchini Yemen tarehe 26 Mach mwaka 2015 kwa lengo la kumrejesha madarakani kibaraka wake, Abdrabbuh Mansur Hadi, rais wa zamani wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kutoroka nchi. Zaidi ya raia elfu 11 wa Yemen wameshauawa na makumi ya maelfu kujeruhiwa, sambamba na mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi katika mashambulizi hayo hadi hivi sasa.

Tags