Israel yafaidika na mkataba wa silaha wa Saudia, Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i29744-israel_yafaidika_na_mkataba_wa_silaha_wa_saudia_marekani
Gazeti moja la Kizayuni, limefichua kuwa, katika mkataba wa mabilioni ya dola wa ununuzi silaha baina ya Marekani na Saudia, mashirika ya Israel yatapata faida kubwa sana.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 29, 2017 03:16 UTC
  • Israel yafaidika na mkataba wa silaha wa Saudia, Marekani

Gazeti moja la Kizayuni, limefichua kuwa, katika mkataba wa mabilioni ya dola wa ununuzi silaha baina ya Marekani na Saudia, mashirika ya Israel yatapata faida kubwa sana.

Televisheni ya Al Alam imenukulu duru za Kizayuni zikisema, mashirika mengi ya uundaji silaha ya Israel yana mikataba na mashirika ya utengenezaji silaha ya Marekani ambayo yanaiuzia Saudia silaha.

Awamu ya kwanza ya Mkataba wa ununuzi silaha uliotowa saini hivi karibuni baina ya Saudia na Marekani wakati Rais Donald Trump alipokuwa mjini Riyadh, itagharimu dola bilioni 110. Mkataba huo unatzamiwa kufika dola biliini 350 katika kipindi cha miaka 10 ijayo.

Taarifa zinasema mkataba huo utapeleeka mashirika ya kutengeneza silaha ya Israel kuweza kupata faida kubwa na yamedhaminiwa faida hiyo kwa muda wa miaka 10.

Ndege ya kivita ya Saudia

Duru za Kizayuni zinadokeza kuwa: "Mashirika ya kuunda zana za kijeshi ya Marekani kama vile  Lockheed Martin ambayo yana jukumu la kuiuzia Saudia silaha na mifumo ya kivita yametakiwa kushirikiana na Shirika la Kuunda Silaha la Israel la Rafael."

Afisa wa Wizara ya Vita ya Israel ambaye hakutaka jina lake litajwe naye pia amesema mkataba mkubwa wa silaha baina ya Marekani na Saudia ni jambo ambalo litaimarisha uwezo wa mashirika ya Israel.

Wakati wa kutiwa saini mkataba huo wa silaha, Rais Donald Trump alitangaza wazi kuwa lengo lake ni kubuni ajira kwa ajili ya Wamarekani huku akijigamba kuwa amefanikiwa kuchukua mabilioni ya dola za fedha za Saudia na kuzipeleka Marekani.