Papa atuma salamu za Ramadhani, akosoa ukaidi wa Trump
(last modified Sat, 03 Jun 2017 07:21:43 GMT )
Jun 03, 2017 07:21 UTC
  • Papa atuma salamu za Ramadhani, akosoa ukaidi wa Trump

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Dunia Papa Francis amekosoa vikali hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kuiondoa nchi yake katika makubaliano ya mabadiliko ya tabianchi yaliyofikiwa mjini Paris, Ufaransa mwaka 2015.

Papa ametumia ujumbe wake wa Ramadhani kwa Waislamu kukosoa hatua hiyo ya Trump, akisisitiza kuwa kazi ya kulinda viumbe vya Mwenyezi Mungu kama mazingira ni jukumu la kila mtu na wala hakuna mtu, serikali au taifa lolote linafaa kutoa tangazo la upande mmoja linaloashiria kuwa na ufahamu zaidi juu ya sayari ya dunia. 

Kwa mtazamo wa rais huyo wa Marekani, suala la ongezeko la joto duniani na mabadiliko ya tabianchi ni mambo yasiyo na ukweli wowote na kwamba eti mambo hayo yamebuniwa tu na Wachina.

Trump alipokutana na Papa huko Vatican hivi karibuni

Papa Francis ametahadharisha katika ujumbe wake huo kuwa: "Iwapo tutaruhusu mtindo wa maisha na baadhi ya maamuzi yetu kuwa na taathira hasi kwa mazingira, basi itakuwa ni kwa madhara na hasara ya wanadamu wote kote duniani." 

Viongozi mbalimbali wa nchi za Magharibi akiwemo Kansela wa Ujerumani  Angela Merkel na mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, wamekosoa vikali uamuzi wa Trump wa kuiondoa Marekani katika Mkataba wa Paris.

Tags