Magaidi wa Taliban waendelea kupata himaya ya nchi za Magharibi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i3238-magaidi_wa_taliban_waendelea_kupata_himaya_ya_nchi_za_magharibi
Balozi wa Uingereza nchini Afghanistan, Dominic Jermey amesema kuwa nchi yake inao uhusiano wa karibu na kundi la kigaidi la Taliban na kwamba ikiwa serikali ya Kabul itahitajia, basi nchi yake inaweza kuutumia uhusiano huo kwa ajili ya kurejesha usalama na amani nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 17, 2016 04:51 UTC
  • Magaidi wa Taliban waendelea kupata himaya ya nchi za Magharibi

Balozi wa Uingereza nchini Afghanistan, Dominic Jermey amesema kuwa nchi yake inao uhusiano wa karibu na kundi la kigaidi la Taliban na kwamba ikiwa serikali ya Kabul itahitajia, basi nchi yake inaweza kuutumia uhusiano huo kwa ajili ya kurejesha usalama na amani nchini humo.

Matamshi ya balozi wa Uingereza mjini Kabul kuhusu uhusiano wa nchi hiyo na Taliban si jambo jipya. Ushirikiano wa Uingereza na Taliban katika Wilaya ya Musa Qala mkoani Helmand nchini Afghanistan ni jambo ambalo limeimarika zaidi kundi hilo na hivyo kutoshambulia wanajeshi wa Uingereza walioko katika mkoa huo. Marekani kidhahiri imebainisha kukasirishwa na uhusiano huo wa Taliban na Uingereza.

Mwaka 2007 aliyekuwa rais wa Afghanistan Hamid Karzai aliwatuhumu Michael Semple na Mervyn Patterson washauri wa zamani wa ngazi za juu na wajumbe wa Umoja wa Mataifa mjini Kabul, Afghanistan ambao wote ni raia wa Uingereza, kuwa walikuwa na mahusiano ya karibu na wanachama wa kundi la Taliban. Karzai aliwatimua Waingereza hao kutoka Afghanistan kutokana na uhusiano waliokwa nao na kundi la Taliban.

Katika kipindi hiki cha kuendelea jitihada za kieneo na kimatiafa kwa jili ya mazungumzo ya kurejesha amani Afghanistan, serikali ya Uingereza inataka maslahi yake yatimizwe na serikali ya Afghanistan na ndio sababu ikasema iko tayari kupatanisha serikali ya Kabil na Taliban. Kwa sasa Marekani na China zinashiriki katika mazungumzo ya pande nne ya kuainisha ramani ya njia ya amani Afghanistan. Pakistan na Uingereza ambazo pia zinashiriki katika mazungumzo hayo zinataka kutumia karata ya turufu katika mchakato wa amani Afghanistan.

Balozi wa Uingereza amejaribu kuonesha kuwa, hamu ya nchi yake kushiriki katika mchakato wa amani Afghanistan inatokana na ombi la Pakistan. Amesema kuwa, Pakistan imeiomba Uingereza iwe na nafasi chanya katika mazungumzo ya amani baina ya Taliban na Afghanistan.

Iwapo madai ya balozi ya Uingereza ni ya kweli, basi tunaweza kusema kuwa Pakistan nayo inataka Afghanistan iikidhie matakwa yake na ili kufikia lengo hilo inamtumia mkoloni wa zamani wa nchi hizo mbili.

Balozi wa Uingereza amedai kuwa London inaweza kuzungumza na pande zinazohasimiana ili ziunge mkono mchakato wa amani Afghanistan. Lakini kile ambacho kimebainika hadi sasa ni kuwa, uingiliaji wa Uingereza katika masuala ya eneo hili ni chanzo cha kukwama mchakato wa amani Afghanistan. Kwa msingi huo iwapo hakutakuwepo uingiliaji wa madola yaliyo nje ya eneo nchi za eneo hilo zinaweza kusaidiana kurejesha amani huko Afghanistan. Hii ni kwa sababu amani Afghanistan itkuwa na maslahi kwa eneo zima na kuendelea vita na mgogoro nchini humo kutakwa na athari mbaya kwa uchumi wa eneo hilo.

Balozi wa Uingereza mjini Kabul amedai kuwa nchi yake inataka kushiriki katika mchakato wa amani Afghanistan katika hali ambayo Marekani imetangaza kuwa haijachukua uamuazi kuhusu kupunguza au kuongeza idadi ya askari wake huko Afghanistan kwa ajili ya kukabiliana na Taliban.

Ingawa Marekani ilitangaza hivi karibuni kuwa wanajeshi wake hawatawashambulia magaidi wa Taliban, lakini kuendelea kuwepo kundi hilo huko Afghanistan ni kisingizio mwafaka kwa Washington kuendele kuikalia kwa mabavu Afghanistan. Nayo Uingereza inatumia fursa hiyo kuendelea kuwa na ushawishi huko Afghanistan na kuishinikiza serikali ya nchi hiyo itekeleze matakwa yake.