Paris: Wafaransa zaidi ya 600 wamejiunga na Daesh
https://parstoday.ir/sw/news/world-i3478-paris_wafaransa_zaidi_ya_600_wamejiunga_na_daesh
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ufaransa imetangaza kuwa Wafaransa zaidi ya 600 wamejiunga na kundi la kigaidi la Daesh katika nchi za Syria na Iraq tangu baada ya mashambulizi ya kigaidi ya Paris Novemba mwaka jana.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 20, 2016 22:29 UTC
  • Paris: Wafaransa zaidi ya 600 wamejiunga na Daesh

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ufaransa imetangaza kuwa Wafaransa zaidi ya 600 wamejiunga na kundi la kigaidi la Daesh katika nchi za Syria na Iraq tangu baada ya mashambulizi ya kigaidi ya Paris Novemba mwaka jana.

Ripoti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ufaransa imesema raia hao wa nchi hiyo walijiunga na kundi la kigaidi la Daesh katika kipindi ambacho mashambulizi dhidi ya kundi hilo la kiwahabi yalikuwa yameshadidi katika nchi za Iraq na Syria. Ripoti hiyo imeongeza kuwa, idadi ya Wafaransa wanaojiunga na kundi la kigaidi la Daesh imeongezeka licha ya serikali ya nchi hiyo kuchukua hatua kali baada ya mashambulizi ya mwaka jana mjini Paris.

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Ufaransa, Manuel Valls ameeleza wasiwasi wake kuhusu wimbi la vijana wa nchi hiyo kujiunga na kundi la kigaidi la Daesh.

Ni vyema kushiria hapa kuwa nchi za Magharibi ikiwemo Ufaransa awali ziliyaunga mkono na kuyasaidia kwa hali na mali makundi ya kigaidi likiwemo la Daesh kwa shabaha ya kuiondoa madarakani serikali halali ya Syria ambayo daima imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono mapambano ya ukombozi wa Palestina dhidi ya utawala ghasibu wa Israel.