Ripoti: Akhari ya mashambulizi ya kigaidi Marekani yanafanywa na Wamarekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i36805-ripoti_akhari_ya_mashambulizi_ya_kigaidi_marekani_yanafanywa_na_wamarekani
Ripoti mpya iliyochapishwa hivi karibuni imebaini kuwa, asilimia 84 ya watu waliofanya mashambulizi ya kigaidi nchini Marekani ni raia wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 26, 2017 00:14 UTC
  • Ripoti: Akhari ya mashambulizi ya kigaidi Marekani yanafanywa na Wamarekani

Ripoti mpya iliyochapishwa hivi karibuni imebaini kuwa, asilimia 84 ya watu waliofanya mashambulizi ya kigaidi nchini Marekani ni raia wa nchi hiyo.

Taasisi ya RAND imesema katika kitabu kilichotayarishwa na Brian Michael Jenkins kwamba, asilimia 84 ya watu waliofanya mashambulizi ya kigaidi katika ardhi ya Marekani wamezaliwa na ni raia wa nchi hiyo.

Jenkins anasema katika kitabu hicho kwamba Marekani, Pakistan, Somalia, Afghanistan kwa mpangilio ndizo zinazoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu waliotekeleza mashambulizi ya kigaidi nchini Marekani. 

Watu wasiopungua 50 waliuawa katika shambulizi ya Las Vegas mapema mwezi uliopita

Katika utangulizi wa kitabu hicho, Brian Michael Jenkins amesema kuwa, baada ya mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001 aghlabu ya mashambulizi ya kigaidi nchini Marekani yamefanywa na watu ambao wamekulia nchini humo lakini hadi sasa hakuna taasisi yoyote yenye misimamo mikali nchini humo ililotambuliwa kuwa ni kundi la kigaidi na kupigwa vita. 

Maafisa wa serikali ya Marekani akiwemo Rais wa nchi hiyo Donald Trump daima wamekuwa wakiweka sheria kali za kuwazuia raia wa nchi za nje kuingia nchi humo kwa kisingizo cha kupambana na ugaidi.