Kufukuzwa wanadiplomasia, zilzala katika diplomasia ya Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i36821-kufukuzwa_wanadiplomasia_zilzala_katika_diplomasia_ya_marekani
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani inapanga mkakati wa kuwafukuza kazi wanadiplomasia wanawake wenye asili ya Kilatini na Kiafrika ikiwa ni katika kuendelezwa hatua za kibaguzi za serikali mpya ya Marekani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 26, 2017 04:18 UTC
  • Kufukuzwa wanadiplomasia, zilzala katika diplomasia ya Marekani

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani inapanga mkakati wa kuwafukuza kazi wanadiplomasia wanawake wenye asili ya Kilatini na Kiafrika ikiwa ni katika kuendelezwa hatua za kibaguzi za serikali mpya ya Marekani.

Taarifa zinasema kuwa, watu wengi kutoka jamii ya waliowachache wamefukuzwa kazi katika Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani katika kipindi hiki cha uongozi wa Rais Donald Trump nchini humo, kitendo ambacho kinamaanisha kufukuzwa kazi wanawake wenye uzoefu na vipawa vya utendaji wenye asili ya Kilatini na Kiafrika. 

Weledi wa mambo wanaamini kuwa uamuzi huo umechukuliwa katika fremu ya kutekeleza siasa za kibaguzi za Donald Trump.  Wachambuzi wa masuala ya kisiasa kwa upande wao wanaamini kuwa, mkakati wa kuwafukuza kazi wanadiplomasia wanawake wenye asili ya Latini na Afrika ambao uliwasilishwa na Rex Tillerson, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani, utaisambaratisha kwa ndani wizara hiyo katika muda wa miezi kadhaa tu.

Rex Tillerson, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani  

Ira N. Forman ambaye alikuwa mwakilishi maalumu wa Marekani katika kusimamia na kukomesha chuki dhidi ya Mayahudi wakati wa utawala wa Obama amesema kuhusiana na suala hilo kuwa: Hatua hizo zinazochukuliwa na Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani zitapelekea kupungua sana wafanyakazi wenye uzoefu ndani ya wizara hiyo.

Vitendo vya kibaguzi vimeripotiwa kuongezeka sana Marekani tangu Donald Trump aliposhika madaraka ya kuiongoza nchi hiyo.