Feb 12, 2018 07:49 UTC
  • Waislamu wazidi kunyanyaswa barani Ulaya; msikiti wachomwa moto Uholanzi

Ikiwa ni katika kuendeleza vitendo vya unyanyasaji dhidi ya Waislamu, watu wenye chuki za kidini wameuchoma moto msikiti mmoja katika mji wa Drachten wa kaskazini mwa nchi hiyo.

Mwandishi wa Radio Tehran amemnukuu Khaled bin Naser, mkurugenzi wa taasisi ya Kiislamu ya mji wa Drachten nchini Uholanzi akisema kuwa, mtu mmoja asiyejulikana, jana Jumapili alivunja vioo vya msikiti huo na kuuchoma moto na kusababisha hasara kubwa kwa msikiti huo.

Amesema, polisi wa mji wa Drachten wamesema kuwa wanafanya uchunguzi wa kugundua waliohusika na shambulio hilo.

Waislamu wa Uholanzi katika maandamano ya kupinga jinai za magaidi wanaotumiwa kuupaka matope Uislamu

 

Tarehe 19 mwezi uliopita wa Januari pia, kundi moja la mrengo wa kulia wenye chuki dhidi ya Waislamu lilishambulia msikiti wa Amir Sultan wa Amsterdam, mji mkuu wa Uholanzi na kubandika mabango yaliyojaa matushi na maneno ya kejeli dhidi ya Waislamu. Inakadiriwa kuwa hivi sasa kuna Waislamu laki tisa katika jamii ya watu milioni 17 ya Uholanzi.

Miezi ya hivi karibuni na hasa baada ya magaidi wa Daesh (ISIS) kufanya mashambulizi katika nchi za Ulaya, makundi yenye chuki na Uislamu yameongeza mashambulizi yao dhidi ya Waislamu na maeneo yao matakatifu hali ambayo imezidi kuwaweka katika hali nguvu Waislamu wa barani Ulaya. 

Cha kushangaza ni kuwa nchi hizo hizo za Magharibi ndizo zilizoanzisha magenge ya kigaidi kama ISIS na kuyaunga mkono na sasa hivi yanatumia vitendo viovu vya magenge hayo yenye majina ya Kiislamu, kuupaka matope Uislamu na kuwanyanyasa na kuwashambulia Waislamu.

Tags