Trump aipigia magoti Iran, aiomba isianzishe tena mradi wake wa nyuklia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i43624-trump_aipigia_magoti_iran_aiomba_isianzishe_tena_mradi_wake_wa_nyuklia
Rais Donald Trump wa Marekani ameiomba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran isianzishe upya mradi wake wa nyuklia, muda mfupi baada ya Rais Hassan Rouhani wa Iran kuionya Washington dhidi ya kukiuka makubaliano ya nyuklia ya Vienna ya mwaka 2015.
(last modified 2026-03-17T04:36:21+00:00 )
Apr 25, 2018 03:19 UTC
  • Trump aipigia magoti Iran, aiomba isianzishe tena mradi wake wa nyuklia

Rais Donald Trump wa Marekani ameiomba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran isianzishe upya mradi wake wa nyuklia, muda mfupi baada ya Rais Hassan Rouhani wa Iran kuionya Washington dhidi ya kukiuka makubaliano ya nyuklia ya Vienna ya mwaka 2015.

Katika mazungumzo yake na mwenzake wa Ufaransa katika Ikulu ya Washington hapo jana, Trump alisema kuwa, iwapo Iran itaanzisha tena miradi yake ya nyuklia, basi itakuwa na matatizo makubwa zaidi ambayo haijawahi kushuhudia.

Moja ya ajenda za Macron nchini Marekani ni kuyanusuru mapatano hayo yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA, ambayo yalianza kutekelezwa Januari mwaka 2016.

Hapo jana Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliionya Marekani dhidi ya kukiuka makubaliano ya nyuklia ya Vienna na kusisitiza kuwa, endapo Washington itajiondoa kwenye mapatano hayo ya kimataifa kama inavyotishia, basi hatua hiyo itakuwa na matokeo mabaya.

Rais Rouhani na maafisa wengine wa ngazi za juu wa serikali ya Iran

Alisema Iran inatekeleza wajibu wake wakati huu kuliko wakati mwingine wowote ule, lakini wale watakaokiuka mapatano hayo wanapaswa kuelewa kuwa, taathira hasi za hatua yao zitawaathiri wao wenyewe.

Naye Dakta Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, chaguo kuu la Iran endapo Marekani itajitoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ni kuanzisha tena shughuli za nyuklia za taifa hili zenye malengo ya amani lakini kwa kiwango cha juu na cha kisasa zaidi.