New York Times: Ufalme wa Marekani unaendelea kuporomoka
Gazeti la New York Times la nchini Marekani limeandika ripoti ya ukosoaji kwamba, Rais Donald Trump wa nchi hiyo anaigeuza Marekani kuwa mbabe ambaye haogopwi tena katika nafsi za upande wa pili.
Ripoti iliyoandikwa na gazeti hilo chini ya kichwa cha maneno yanayosema 'Kuporomoka Ufalme wa Marekani' imefafanua kuwa, serikali ya Washington kupitia siasa rasmi inawatenganisha watoto na wazazi wao na kisha kuwafunga, huku viongozi wa nchi hiyo wakisisitiza kwamba sio jela bali wanawahifadhi tu. Katika ripoti hiyo kumeelezwa kwamba kwa upande mmoja Rais Donald Trump alitaka kusimamishwa uchunguzi wa Polisi ya Federali ya Marekani (FBI) kuwahusu wasaidizi wake huku badala yake akisisitizia umuhimu wa kufuatiliwa maadui na wapinzani wake wa kisiasa.
Limeongeza kwa kusema kuwa, kuibuka kwa mapigano ya kimpaka, kushambuliwa haki ya kujitawala ndani ya nchi, kuvunjiwa heshima viongozi wa kidemokrasia na kuwakumbatia madikteta na kadhalika uvunjaji wa mikataba ya kimataifa na kibiashara, yote hayo yanabainisha ni kwa namna gani serikali ya Marekani isivyozingatia matukufu. New York Times sambamba na kubainisha kwamba Marekani haikuwa na nguvu katika kipindi cha miaka 70 iliyopita, limeandika kwamba Trump yuko katika kuweweseka na anafanya makosa kwa kudhani kwamba nchi nyingine zitajisalimisha kwake kwa kutumia vitisho.