Uturuki nayo yaingia katika vita vya Kiuchumi dhidi ya Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i46140-uturuki_nayo_yaingia_katika_vita_vya_kiuchumi_dhidi_ya_marekani
Katika radiamali yake kufuatia hatua ya Marekani ya kuzipandishia ushuru bidhaa zinazozalishwa Uturuki, serikali ya Ankara imechukua hatua sawa na ya China na Umoja wa Ulaya ya kuingia katika vita vya biashara dhidi ya Washington.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 21, 2018 09:15 UTC
  • Uturuki nayo yaingia katika vita vya Kiuchumi dhidi ya Marekani

Katika radiamali yake kufuatia hatua ya Marekani ya kuzipandishia ushuru bidhaa zinazozalishwa Uturuki, serikali ya Ankara imechukua hatua sawa na ya China na Umoja wa Ulaya ya kuingia katika vita vya biashara dhidi ya Washington.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Uchumi ya Uturuki imesema kuwa, kuanzia leo Alkhamisi serikali ya nchi hiyo itaanza kutekeleza hatua mkabala za kiuchumi dhidi ya Marekani kwa kuzipandishia ushuru wa zaidi ya dola milioni 266 bidhaa za Marekani zinazoingizwa nchi hiyo. Sambamba na kuitaja hatua ya Marekani kuwa isiyo ya mantiki kwa kuingia katika vita vya kibiashara na nchi tofauti za dunia, imeongeza kuwa hatua za ulipizaji kisasi za Uturuki dhidi ya Washington zinajumuisha bidhaa tofauti za Marekani zinazoingizwa Uturuki kuanzia magari, mashine za viwandani na bidhaa za petrokemikali.

Waziri wa Uchumi wa Uturuki.

Mwezi Machi mwaka huu, Rais Donald Trump wa Marekani alichukua uamuzi wa kupandisha kwa asilimia 10 hadi 25 ushuru dhidi ya bidhaa za chuma ya pua na aluminiamu. Maamuzi hayo yalikosolewa vikali na nchi tofauti za dunia huku nchi kadhaa zikitangaza rasmi kuingia vitani na Washington katika sekta ya biashara.