Marekani ni miongoni mwa nchi hatari zaidi kwa wanawake
https://parstoday.ir/sw/news/world-i46334-marekani_ni_miongoni_mwa_nchi_hatari_zaidi_kwa_wanawake
Marekani imetajwa kuwa miongoni mwa nchi hatari zaidi kwa wanawake duniani ambapo imebainika kuwa katika kila wanawake watano nchini humo mmoja wao amewahi kunajisiwa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 26, 2018 02:58 UTC
  • Marekani ni miongoni mwa nchi hatari zaidi kwa wanawake

Marekani imetajwa kuwa miongoni mwa nchi hatari zaidi kwa wanawake duniani ambapo imebainika kuwa katika kila wanawake watano nchini humo mmoja wao amewahi kunajisiwa.

Katika uchunguzi uliofanywa na Taasisi ya Thomson Reuters, Marekani iko katika orodha ya nchi 10 hatari zaidi dunaini miongoni mwa nchi zote 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa.

India imetajwa kuwa nchi hatari zaidi kwa wanawake ikifuatiwa na Afghanistan na Syria nchi ambazo zinakabiliwa na wimbi la mashambulizi ya magaidi wakufurisaji ambao wanapata himaya ya nchi za Magharibi na waitifaki wao katika.

Wanaharakati wa kijamii wameanzisha harakati za kuwalinda wanawake Marekani kutokana na ongezeko la kasi la vitendo vya kuwanajisi mara kwa mara au kuwadhalilisha kijinsia wakiwa kazini.

Mwaka jana waigizaji filamu wengi wa kike katika kituo cha Hollywood walimshutumu mtayarishaji filamu Harvey Weinstein kwa unyanyasaji wa kijinsia. 

Hayo yanajiri wakati ambao Marekani imekuwa ikijinadi kuwa eti ni mtetezi wa haki za wanawake duniani.