Waziri kivuli wa Uingereza: Donald Trump ni mbaguzi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i53941-waziri_kivuli_wa_uingereza_donald_trump_ni_mbaguzi
Waziri kivuli wa mambo ya nje wa Uingereza amemkosoa vikali Rais Donald Ttump wa Marekani na kumtaja kuwa ni mbaguzi na muwindaji wa ngono.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 05, 2019 22:01 UTC
  • Waziri kivuli wa Uingereza: Donald Trump ni mbaguzi

Waziri kivuli wa mambo ya nje wa Uingereza amemkosoa vikali Rais Donald Ttump wa Marekani na kumtaja kuwa ni mbaguzi na muwindaji wa ngono.

Emily Thornberry amepinga vikali safari ya sasa ya Rais wa Marekani nchini Uingereza na kusema: "Safari rasmi ya kiserikali ni jambo la fahari na kujivunia lakini hatudhani kuwa rais huyo wa Marekani anastahiki fahari hiyo."

Thornberry amesema kuwa, 'Rais wa Marekani ni muwindaji wa ngono na mbaguzi wa rangi na tunapaswa kujadili ni kwa nini Uingereza imetishika kiasi hiki; kwa nini tunashindwa kusema mambo haya?, amehoji waziri kivuli wa mambo ya nje wa Uingereza

Vilevile ameunga mkono uamuzi uliochukuliwa na kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Leba, Jeremy Corbyn wa kususia safari ya Donald Trump nchini Uingereza. 

Maelfu ya waandamanaji wakipinga safari ya Trump nchini Uingereza

Corbyn mbaye ni kiongozi wa chama chenye wafuasi wengi zaidi nchini Uingereza amekuwa akitangaza mara kwa mara upinzani wake dhidi ya siasa za Rais wa Marekani na amejiunga na waandamani wanaopinga safari ya Donald Trump nchini humo.

Trump aliwasili London Jumatatu iliyopita kwa safari rasmi ya siku tatu katikati ya wimbi kubwa la malalamiko na maandamano ya makumi ya taasisi za kiraia. jumuiya za kutetea haki za binadamu, mashirika yanayopinga vita na ubaguzi na taasisi zinazopinga silaha za nyuklia.