Mwandishi wa habari asema Trump alimbaka miaka ya 1990
https://parstoday.ir/sw/news/world-i54283-mwandishi_wa_habari_asema_trump_alimbaka_miaka_ya_1990
Rais Donald Trump wa Marekani anaandamwa na kashfa nyingine ya ufuska baada ya mwanadishi wa habari kwa jina E. Jean Carroll, kufichua kuwa kiongozi huyo wa Marekani wakati huo akiwa mjasiriamali alimbaka katikati ya miaka 90.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 22, 2019 08:42 UTC
  • Mwandishi wa habari asema Trump alimbaka miaka ya 1990

Rais Donald Trump wa Marekani anaandamwa na kashfa nyingine ya ufuska baada ya mwanadishi wa habari kwa jina E. Jean Carroll, kufichua kuwa kiongozi huyo wa Marekani wakati huo akiwa mjasiriamali alimbaka katikati ya miaka 90.

Madai ya mwanabahari huyo ambaye pia ni mwandishi wa vitabu yamechapishwa katika toleo la jana Ijumaa la Jarida la New York. 

Mwanamke huyo amesema tukio hilo lilitokea ima mwishoni mwa mwaka 1995 au mwanzoni mwa mwaka 1996, ambapo Trump alimdhalilisha kigono wakiwa katika jengo la Bergdorf Goodman mjini Manhattan, licha ya kuwa yeye Trump alikuwa ameoa mke kwa jina Marla Maples.

Trump kupitia Ikulu ya White House amekanusha madai hayo na kusisitiza kuwa mwandishi huyo ameyaibua hayo ili kukitafutia soko kitabu chake kipya.

Kashfa za ngono na matamshi ya ufuska yamemfanya Trump kuwa mmoja wa marais wasio na maadili nchini Marekani katika zama hizi.

Trump na mcheza filamu za ngono, Stormy Daniels

Mwaka jana, Trump baada ya kukanusha kwa muda mrefu, alisadikisha kuwa alimlipa wakili wake binafsi Michael Cohen, fedha za kifumbamdomo dola laki moja na elfu thelathini ambazo wakili huyo alimpatia muigizaji wa filamu chafu za ngono maarufu kwa jina la Stormy Daniels ili asifichue kuhusu uhusiano wao.

Mnamo mwezi Februari mwaka jana, sambamba na kutimia miaka miwili ya urais wa Marekani, mamia ya maelfu ya wanawake waliandamana katika kila pembe ya Marekani dhidi ya kiongozi huyo.