Carter: Vita vyote vya Marekani havijakuwa na manufaa
https://parstoday.ir/sw/news/world-i54360-carter_vita_vyote_vya_marekani_havijakuwa_na_manufaa
Rais wa zamani wa Marekani amekiri kuwa vita vyote vilivyoendeshwa na Marekani hadi kufiki sasa havijakuwa na udharura wala manufaa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 25, 2019 22:22 UTC
  • Carter: Vita vyote vya Marekani havijakuwa na manufaa

Rais wa zamani wa Marekani amekiri kuwa vita vyote vilivyoendeshwa na Marekani hadi kufiki sasa havijakuwa na udharura wala manufaa.

Akihutubia katika kanisa la Maranatha Baptis huko Georgia, Jimy Carter  amesema kuwa pamoja na kujihesabu sisi kuwa ni Wakristo lakini tunatambulika duniani kote kama nchi inayopenda sana vita ulimwenguni. Rais wa zamani wa Marekani ameongeza kusema kuwa na hapa ninamnukuu" mimi ninaamini kuwa katika vita vyote ambavyo tumeshiriki havikuwa na udharura". Carter amebainisha kuwa anakubaliana na uamuzi wa Trump wa kuzuia kuchukua hatua ya kijeshi dhidi ya Iran na hafikirii vita kama hivyo na kwa kiujumla vita vyote vya karibuni ni vya kimantiki.  

Alhamisi tarehe 20 mwezi huu ndege ya kijasusi ya Marekani aina ya RQ- 4A Global Hawk ilikiuka anga ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika eneo la Kuhe Mubarak katika mkoa wa Hormozgan na kutunguliwa na  kikosi cha anga cha jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH). Baada ya kutunguliwa droni hiyo ya kijasusi ya Marekani; Rais wa nchi hiyo Donald Trump alitoa matamshi yenye kutatanisha ambapo awali alisema kuwa alikuwa amekusudia kuishambulia Iran lakini akafutilia mbali suala hilo. Hata hivyo baadaye alisema kuwa shambulio dhidi ya Iran halijatupiliwa mbali, bali muda wake umeakhirishwa.

Mabaki ya ndege ya kijasusi ya Marekani iliyotunguliwa na Iran

Akijibu matamshi na msimamo huo wa White House, Sayyid Abbas Musavi Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa taifa la Iran linajibu udiplomasia kwa udiplomasia, heshima kwa heshima, na vita kwa kujilinda na kujitetea kwa nguvu zake zote.