Uchunguzi wa maoni: Wamarekani wamechoshwa na mitazamo ya Donald Trump
https://parstoday.ir/sw/news/world-i54538-uchunguzi_wa_maoni_wamarekani_wamechoshwa_na_mitazamo_ya_donald_trump
Uchunguzi mpya wa maoni unaonesha kuwa, wananchi wa Marekani wamechoshwa na mitazamo ya Rais wa nchi hiyo, Donald Trump.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 04, 2019 01:50 UTC
  • Uchunguzi wa maoni: Wamarekani wamechoshwa na mitazamo ya Donald Trump

Uchunguzi mpya wa maoni unaonesha kuwa, wananchi wa Marekani wamechoshwa na mitazamo ya Rais wa nchi hiyo, Donald Trump.

Matokeo ya uchunguzi mpya uliofanywa na taasiisi ya PEW kuhusu msimamo wa Wamarekani mkabala wa mitazamo ya Donald Trump yanaonesha kuwa, asilimia 67 ya Wamarekani wamechoshwa na matamshi yake na asilimia 75 wana wasiwasi kuhusiana na mitazamo ya kiongozi huyo. 

Matokeo hayo ya maoni yaliyotangazwa jana yanaonesha kuwa, asilimia 69 ya Wamarekani wanaona aibu kutokana na maneno na matamshi ya Donald Trump na asilimia 65 wanasema wanakasirishwa na mitazamo yake. 

Donald Trump

Vilevile asilimia 62 ya wananchi wa Marekani wanahisi kuwa matamshi yanayotolewa na rais wa nchi yao "yanawadhalilisha". 

Rais Donald Trump wa Marekani amekuwa akivishambulia vyombo vya habari vinavyomkosoa au kuchapisha habari zinazomhusu na badala yake anajigamba kuwa ndiye Rais anayependwa zaidi katika historia ya Marekani! Hii ni licha ya kwamba, chunguzi zote za maoni zinaonesha kuwa, Trump ndiye anayechukiwa zaidi na idadi kubwa ya Wamarekani baina ya marais wote waliotangulia wa Marekani.