Sanders: Trump ni Rais hatari zaidi katika historia ya Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i63389-sanders_trump_ni_rais_hatari_zaidi_katika_historia_ya_marekani
Seneta wa jimbo la Vermont nchini Marekani ametaka kuungana wananchi wa Marekani ili kutoa pigo kwa Rais wa sasa wa nchi hiyo Donald Trump ambaye amemtaja kuwa ni rais hatari zaidi wa Marekani kuwahi kushuhudiwa katika historia ya nchi hiyo.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Sep 12, 2020 22:46 UTC
  • Sanders: Trump ni Rais hatari zaidi katika historia ya Marekani

Seneta wa jimbo la Vermont nchini Marekani ametaka kuungana wananchi wa Marekani ili kutoa pigo kwa Rais wa sasa wa nchi hiyo Donald Trump ambaye amemtaja kuwa ni rais hatari zaidi wa Marekani kuwahi kushuhudiwa katika historia ya nchi hiyo.

Bernie Sanders  jana Jumamosi alituma ujumbe katika ukurasa wake wa twitter akitaka kuungana wananchi wa Marekani ili kutoa pigo kwa Rais Donald Trump wa nchi hiyo. Huko nyuma pia, Sanders alimtaja rais huyo wa Marekani kama mtu mwenye fikra za kibeberu ambaye anafanya kila awezalo kudhoofisha na kuangamiza demokrasia. 

Ikiwa imesalia miezi chini ya miwili hadi kufanyika uchaguzi wa Rais huko Marekani; chunguzi mbalimbali za maoni zilizofanywa nchini humo zinaonyesha kuwa, Joe Biden mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha Democrat ana uungaji mkono zaidi miongoni mwa fikra za waliowengi nchini humo. Hali hiyo imetokana na utendaji mbovu wa Trump katika miezi ya karibuni. 

Joe Biden, mgombea kiti cha urais Marekani wa chama cha Democrat 

Utendaji dhaifu wa Rais Trump katika kushughulikia maambukizi ya corona na matamshi yake yenye kukinzana kuhusu maandamano na malalamiko ya wananchi huko Marekani yote hayo yamepelekeanimiongoni mwa sababu zlizosababisha kupunguza uungaji mkono wa wananchi kwake.