Trump: Biden hatakuwa rais halali
https://parstoday.ir/sw/news/world-i65184-trump_biden_hatakuwa_rais_halali
Ikiwa ni katika kuendeleza propaganda zake za kutilia shaka matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwaka huu nchini Marekani na kujaribu kufunika fedheha ya kushindwa kwake katika uchaguzi huo, Rais Donald Trump wa Marekani amedai kwamba Joe Biden aliyeshinda uchaguzi huo hatakuwa rais halali wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Dec 14, 2020 06:53 UTC
  • Trump: Biden hatakuwa rais halali

Ikiwa ni katika kuendeleza propaganda zake za kutilia shaka matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwaka huu nchini Marekani na kujaribu kufunika fedheha ya kushindwa kwake katika uchaguzi huo, Rais Donald Trump wa Marekani amedai kwamba Joe Biden aliyeshinda uchaguzi huo hatakuwa rais halali wa nchi hiyo.

Akijibu swali aliloulizwa na waandishi habari kuhusu kile kitakachotokea iwapo hatakuwa amekiri kushindwa na Biden kufikia wakati wa kuapishwa kwake kama rais wa Marekani, Trump ambaye wiki iliyopita alipata mapigo mengine mawili ya kisheria katika majimbo ya Pennsylvania na Texas baada ya Mahakama ya Juu ya Marekani kutupilia mbali madai yake ya kufanyika udanganyifu katika uchaguzi, amesema kuwa Biden hatakuwa rais halali wa nchi hiyo.

Trump ametoa madai hayo katika hali ambayo jana Jumapili, Mahakama Kuu ya Jimbo la Georgia ilitupilia mbali ombi lake lililowasilishwa mahakamani na timu yake ya mawakili wakitaka matokeo ya uchaguzi katika jimbo hilo yafutiliwe mbali.

Joe Biden aliyeshinda uchaguzi wa mwaka huu wa rais wa Marekani

Jumamosi pia jaji wa serikali kuu katika jimbo la Wisconsin alitupilia mbali ombi kama hilo la Trump kutaka matokeo ya uchaguzi katika jimbo hilo yabatilishwe.

Jimbo la Wisconsin tayari limethibitisha ushindi wa Biden mgombea wa chama cha Democrat kuwa rais mteule wa Marekani. Hii ni katika hali ambayo Trump alishinda uchaguzi mkuu katika jimbo hilo mwaka 2016. Gavana wa jimbo hilo ametangaza kuwa uchaguzi uliofanyika katika jimbo hilo ulikuwa salama, wa haki na wa kuaminika.