Mar 31, 2021 07:11 UTC
  • Kansela wa Austria akososa

Kansela Sebastain Kurz wa Austria ameutuhumu Umoja wa Ulaya kuwa haugawi kwa uadilifu chanjo ya corona na kueleza kwamba nchi yake iko kwenye mazungumzo na Russia ya kununua dozi milioni moja za chanjo iliyotengenezwa na nchi hiyo ya Sputnik V.

Kansela Kurz ameutuhumu Umoja wa Ulaya kuwa unacheza mchezo mchafu katika ugavi wa chanjo ya corona kwa nchi mbali mbali na kuongeza kuwa ameshafanya mazungumzo na Russia kwa ajili ya kununua dozi milioni moja za chanjo ya Sputnik V.

Kansela wa Austria amesema, tangu mwezi Februari wamekuwa na mashauriano mazuri na Russia kwa ajili ya kupatiwa chanjo ya Sputnik na akasisitiza: "Unapofika wakati wa utoaji chanjo kusiwepo na suala lolote la jiopolitiki ; kitu muhimu pekee ni kuona kama chanjo iliyopo ni athriifu na si hatarishi au la."

Chanjo ya Corona ya Sputnik V

Kurz ameongeza kuwa, ikiwa Austria itapokea dozi za ziada milioni moja za chanjo itawezekana nchi hiyo kurejea haraka katika mazingira ya kawaida.

Mara kadhaa Kansela huyo wa Austria ameonyesha uungaji mkono wake kwa chanjo ya Sputnik V iliyotengenezwa Russia na kuutaka Umoja wa Ulaya utoe idhini haraka iwezakanavyo kwa nchi zingine kutumia chanjo hiyo kwa dharura.

Tarehe 26 Februari, Rais Vladimir Putin wa Russia na Kansela Sebastian Kurz wa Austria walifanya mazungumzo kwa njia ya simu kuhusu jitihada za pamoja zinazopasa kufanywa kwa ajili ya kupambana na usambaaji wa virusi vya corona na kuipatia Austria chanjo ya Sputnik V iliyotengenezwa Russia.../  

Tags