May 22, 2024 10:27 UTC
  • Putin: Kifo cha Raisi ni pigo kubwa; nitaendelea kuimarisha uhusiano na Iran

Rais Vladimir Putin wa Russia ameeleza kusikitishwa na kuhuzunishwa sana na kifo cha Rais Ebrahim Raisi wa Iran na kusema ni pigo kubwa kwa taifa.

Putin ameeleza haya katika mkutano na Spika wa Bunge la Russia (Duma) Vyacheslav Volodin mjini Moscow. 'Kifo cha Rais Raisi ni pigo kubwa, kwanza kabisa kwa Iran na watu wake. Alikuwa mshirika wa kutegemewa sana, mtu wa moja kwa moja, anayejiamini, ambaye alikuwa na ari ya kutetea maslahi ya taifa lake," amesema Putin.

Rais wa Russia pia amemuelezea mwendazake Rais wa Iran kuwa shakhsia mwenye msimamo madhubuti. "Pale tulipokuwa tukiafikiana naye kutekeleza jambo fulani mara zote tulikuwa na uhakika kwamba makubaliano yetu yote yatatetelezwa." 

Shahidi Rais Ebrahim Raisi 

Rais Putin ameendelea kubainisha kuwa Moscow ipo tayari kuendeleza ushirikiano na Iran sawa kabisa na ilivyokuwa chini ya uongozi wa Ebrahim Raisi na kuahidi kuwa atafanya kila awezalo kuhakikisha kuwa uhusiano kati ya Russia na Iran unaimarika kama ilivyokuwa wakati wa uongozi wa Raisi. 

Nchi nyingi khususan nchi jirani na Iran zimetangaza siku kadhaa za maombolezo kuwaenzi shahidi Rais Ebrahim Raisi na mashahidi wenzake. 

Shahid Sayyid Raisi atazikwa kesho katika mji mtakatifu wa Mash'hadi alikozaliwa. 

Tags