Umoja wa Ulaya waendelea kuingilia masuala ya ndani ya Afghanistan
https://parstoday.ir/sw/news/world-i73592-umoja_wa_ulaya_waendelea_kuingilia_masuala_ya_ndani_ya_afghanistan
Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya ameingilia tena masuala ya ndani ya Afghanistan sambamba na kufumbia jicho jinai zilizofanywa na Marekani na waitifaki wake wa Ulaya nchini Afghanistan.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 17, 2021 02:34 UTC
  • Umoja wa Ulaya waendelea kuingilia masuala ya ndani ya Afghanistan

Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya ameingilia tena masuala ya ndani ya Afghanistan sambamba na kufumbia jicho jinai zilizofanywa na Marekani na waitifaki wake wa Ulaya nchini Afghanistan.

Josep Borrell amedai kuwa kuna haja ya kurejeshwa usalama huko Afghanistan na kwamba jamii ya kimataifa inazitolea mwito pande zinazozozana nchini humo kuwawezesha raia wa kigeni na wa Waafghani kuondoka nchini humo kwa amani.  

Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya ameongeza kuwa, kesho Jumanne Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa umoja huo wafanyanya mkutano kwa njia ya intaneti kujadili hali ya mambo ya Afghanistan. 

Bila ya kuashiria jinai za Marekani na waitifaki wake wa Ulaya huko Afghanistan sambamba na kuongezeka mashambulizi ya kundi la Taliban nchini humo, Borrel ametaka kusitishwa mara moja mashambulizi ya Taliban.  

Zaidi ya nchi 60 duniani zimetoa taarifa ya pamoja na kueleza kuwa raia wa nchi za nje na Waafghani wanaotaka kuondoka nchini Afghanistan wanapasa kuruhusiwa kuondoka na viwanja vya ndege na vivuko vya mipakani vinapasa kufunguliwa na kubakia wazi. Idadi kubwa ya wananchi wa Kabul wamevamia uwanja wa ndege wa Kabul wakitaka kukimbia nchi baada ya kundi la Taliban kuiudhibiti miji kadhaa ya nchi hiyo ukiwemo mji mkuu, Kabul.

Waafghani katika harakati za kuikimbia nchi 

Imeelezwa kuwa wanajeshi wa Marekani wamewazuia wananchi wa Afghanistan waliokuwa wakijaribu kupanda ndege za Marekani na kuikimbia nchi na kwamba wanajeshi wa Marekani wamewafyatulia risasi raia hao katika uwanja wa ndege wa Kabul na kuuwa watu wanne. Imeelezwa kuwa, ndege za kijeshi zinazotoka Kabul ni mahsusi kwa jaili ya kuwasafirisha wanadiplomasia na wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani.