Baraza la Ulaya latahadharisha kuhusu hali mbaya ya wafungwa nchini Ufaransa
https://parstoday.ir/sw/news/world-i74790-baraza_la_ulaya_latahadharisha_kuhusu_hali_mbaya_ya_wafungwa_nchini_ufaransa
Baraza la Ulaya limetahadharisha kuhusu hali mbaya ya wafungwa katika jela za Ufaransa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 18, 2021 03:26 UTC
  • Baraza la Ulaya latahadharisha kuhusu hali mbaya ya wafungwa nchini Ufaransa

Baraza la Ulaya limetahadharisha kuhusu hali mbaya ya wafungwa katika jela za Ufaransa.

Kamati ya Mawaziri ya Baraza la Ulaya jana Ijumaa iliitaka serikali ya Ufaransa kuboresha hali ya wafungwa katika jela za nchi hiyo na kutumia stratijia ya kupunguza msongamano wa wafungwa katika jela hizo.

Kamati hiyo ilikutana siku za tarehe 14 na 16 mwezi huu wa Septemba kwa ajili ya kuchunguza hukumu za Mahakama ya Haki za Binadamu ya Ulaya kuhusu tatizo la kimuundo la msongamano wa wafungwa na hali mbaya ya mahabusu katika jela nyingi za Ufaransa. Mwezi Januari mwaka jana pia kulitolewa ripoti za mienendo mibaya dhidi ya makumi ya wafungwa katika jela za miji ya Nice, Nîmes, Fresnes, Diocese, Baie-Mahault ‌na Fanotania.

Kamati hiyo pia imewataka maafisa wa serikali ya Paris kuchukua hatua za haraka za kuboresha mazingira ya wafungwa na kutekeleza stratijia ya muda mrefu kwa ajili ya kupunguza msongamano wa wafungwa ndani ya jela za nchi hiyo.