Russia yazitambua rasmi Jamhuri za Donetsk na Luhansk kama nchi huru
https://parstoday.ir/sw/news/world-i80638-russia_yazitambua_rasmi_jamhuri_za_donetsk_na_luhansk_kama_nchi_huru
Rais Vladimir Putin wa Russia ametangaza kuwa Moscow imetambua rasmi uhuru wa Jamhuri za watu wa Donetsk na Luhansk na tayari amesaini mikataba ya ushirikiano na urafiki na viongozi wa jamhuri mbili hizo katika ikulu ya Kremlin.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 22, 2022 03:41 UTC
  • Russia yazitambua rasmi Jamhuri za Donetsk na Luhansk kama nchi huru

Rais Vladimir Putin wa Russia ametangaza kuwa Moscow imetambua rasmi uhuru wa Jamhuri za watu wa Donetsk na Luhansk na tayari amesaini mikataba ya ushirikiano na urafiki na viongozi wa jamhuri mbili hizo katika ikulu ya Kremlin.

Leonid Ivanovich Pasechnik kiongozi wa Jamhuri ya Donetsk na mwenzake wa Luhansk Denis Vladimirovich Pushilin jana Jumatatu walimuomba Rais Vladimir Putin wa Russia ayatambue rasmi maeneo hayo maawili kama nchi zilizo huru. Wiki iliyopita, bunge la Russia (Duma) pia liliwaslisha ombi kwa Rais Putin likimtaka atambue rasmi kuwa huru eneo la Donbass linalotaka kujitenga na Ukraine. 

Eneo la Donbass huko mashariki mwa Ukraine linajumuisha maeneo ya Donetsk na Luhansk na pia maeneo mengine kadhaa yanayokaliwa na raia wenye asili ya Russia. Maeneo ya Donetsk na Luhansk mwaka 2014 yalitangaza kwa upande mmoja kuwa huru kutoka Kiev baada ya kubadilika utawala huko Ukraine. 

Shirika la habari la Iran, Irna limeripoti kuwa, Rais Putin jana alasiri alihutubu na kutangaza kuyatambua rasmi maeneo hayo mawili; ambapo aliashiria pia historia ya kuasisiwa taifa la Ukraine na uhusiano wa karibu sana na nchi hiyo katika miaka kadhaa ya karibuni. Rais wa Russia alisema: Ukraine ilipewa maeneo ya kihistoria ya Russia katika zama za umoja wa Kisovieti, na haijulikani kwa nini hatua hiyo ilitekelezwa. 

Rais Vladimir Putin wa Russia